Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Waliona Uchungu Lakini Hawakuachwa

  Lakini walikuwa wameelekea kutiwa uchungu mara ya pili kwa ajili ya kutopata yaliyotazamiwa. Wakati ule waliokuwa wakimtazamia Mwokozi ulipita, naye hakuonekana. Walikuwa wamermgoja wakiwa na tumaini kuu lililo thabiti, lakini wakati ule wakawa kama Mariamu, alipofika kwenye kaburi la Yesu na kulikuta li wazi, akapaaza sauti akilia, “Wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.” Yohana 20:13.VK 72.1

  Hali ya kicho, na woga ya kwamba labda ujumbe ule uliweza kuwa wa kweli, kwa muda fulani ilikuwa imewazuia walimwengu wasioamini. -Lakini hali hii haikutoweka mara moja baada ya kupita kwa wakati ule watu wale walioona uchungu, lakini kwa jinsi ambavyo hawakuona dalili yo yote iliyoonyesha ghadhabu ya Mungu, waliacha woga wakaanza tena kuwafanyiziav mzaha na lawama. Watu wengi waliokuwa wakijidai ya kwamba waliamini ya kuwa marejeo ya. Bwana yalikaribia, walnkanusha imani yao. Wengine ambao walikuwa na hakika zaidi, waiiona uchungu sana kwa jinsi walivyoona wameferheheshwa, hata wakataka kupotea usoni,.pa dunia. Waltmnung’unikia Mungu kama Yana alivyofanya, waiiona afadhali kufa kuliko kuishi. Wale waliokuwa wameijenga imani yao juu ya maoni ya wenzao badala ya Neno la Mungu, sasa walikuwa tayari tena kuyageuza maoni yao. Wenye kudhihaki waliwavuta wanyonge na waoga wakawafuata, na wote wakaungama kwa kutangaza ya kwamba haiwapasi kuogopa wala kumngoja Bwana tena. Wakati ulikuwa umepita, wala Bwana hakuja, na walifikiri ya kwamba dunia ingedumu kuwa katika hali ile kwa miaka elfu nyingi.VK 72.2

  Waaminio wenye bidii walikuwa wameacha vyote kwa ajili ya Kristo, na walikuwa wamefahamu kuwapo kwake kati yao zaidi ya zamani. Walidhani ya kwamba wamelitoa onyo la mwisho kwa dunia yote, na walikuwa wakitazamia kupokewa na Bwana wao karibuni na kukaa pamoja naye na malaika za mbinguni; na kwa kadiri kubwa walikuwa wametengana na lile kundi la watu wasioamini. Walikuwa wameomba kwa makini, “Uje Bwana Yesu, uje upesi.” Lakini hakuja. Waliona ya kwamba kuanza tena kuuchukua mzigo wa masumbufu ya dunia hii na mashaka, na kuvumilia dhihaka> dharau, na matusi ya watu wa dunia, kweli kulikuwa majaribu ya imani na uvumilivu.VK 73.1

  Walakini uchungu huo haukuwa mkuu kama ule uliowapata wanafunzi wa Kristo wakati wa kuja kwake mara va kwanza. Yesu alipoingia Yerusalemu kwa shangwe akimpanda punda, wafuasi wake walidhani ya kwamba alikuwa karibu kuketi katika kiti cha enzi cha Daudi na kuwaokoa Waisraeli mikononi mwa watesi wao. Kwa furaha kuu na matumaini, walishindana wao kwa wao kwa kumheshimu Mfalme wao. Watu wengi waliyatandaza mavazi yao njiani yapate kuwa kama zulia atakapopitia, na wengine wakakata matawi ya miti wakayatandaza njiani. Kwa furaha kuu walipaaza sauti wakisema. “Hosana, mwana wa Daudi!”VK 73.2

  Mafarisayo, waliposhtushwa na kukasirishwa na kelele hii ya shangwe, wakamwomba Yesu awakaripie wanafunzi wake, na Yesu akawajibu akisema, “Wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.” Luka 19:40. Unabii ni lazima utimizwe. Wanafunzi walikuwa wakilitimiza kusudi la Mungu; lakini walikuwa wanaelekea kuona uchungu mkuu ajabu. Zilipita siku chache tu ndipo walimwona Mwokozi akifa kifo cha maumivu makuu, wakamzika kaburini. Mambo waliyoyatazamia yalikuwa hayajatimizwa hata kidogo, na matumaini yao yalikufa pamoja na Yesu. Bwana wao alipofufuka akiwa mshindi, kutoka katika wafu, ndipo walipofahamu ya kwamba yale yote yalikuwa yametabiriwa na manabii ya kwamba “ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu.” Matendo 17:3. Vivyo hivyo maneno ya unabii yalitimizwa katika ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili. Ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili ulitolewa kwa wakati uliopangwa, na habari hizo zilitimiliza kazi ambayo Mungu alikusudia kutimiza.VK 73.3

  Watu wa dunia walikuwa wakitazama, wakingoja waone jambo litakalotendeka. na wakiona ya kwamba wakati umepita, wala Kristo hakuonekana, ndipo mambo hayo yote na mafundisho hayo yote juu ya kumtazamia Kristo yangeachwa kabisa. Ingawa wengi walipojaribiwa vikali waliacha imani yao, lakini kulikuwa na wengine waliosimama imara. Hawakulivumbua kosa lo lote kwa vile walivyohesabu miaka iliyoandikwa katika unabii. Adui zao wenye akili kabisa hawakuweza kupindua maneno hayo jinsi walivyohesabu wakati. Kwa kweli, kulikuwa na kosa kwa jambo lililotazamiwa hasa, lakini neno hilo halikuweza kuipunguza imani yao juu ya Neno la Mungu.VK 74.1

  Mungu hakuwaacha watu wake; Roho wake alidumu kuwa na wale ambao hawakuikataa kwa haraka ile nuru waliyokwisha kuipokea, na kuinenea habari ya marejeo ya Kristo. Mtume Paulo, alipokuwa akivitazama vizazi vya mbele, aliandika maneno ya kuwaonya na kuwatia nguvu wanaojaribiwa, maneno yaliyofaa kwa wale waliomngojea Bwana katika siku zile za taabu: “Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.” Ebr. 10:35-39.VK 75.1

  Njia yao ya pekee ya usalama ilikuwa tu kuikuza ile nuru ambayo walikuwa wamepewa na Mungu, kuzishikilia ahadi zake, kudumu kuyachungua Maandiko, na kumngoja kwa saburi wakitazamia kuipokea nuru zaidi.VK 75.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents