Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya Pili - Siri Ya Kuasi

  *****

  MTUME Paulo, katika barua yake ya pili kwa Wathesalonike, aliuagua uasi mkuu ambao mwishowe ungetokea utawala wa Kanisa la Kirumi. Alisema dhahiri ya kwamba siku ya Kristo haitakuja “usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafai yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.” Zaidi ya haya, natume awaonya ndugu zake ya kwamba ile“siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi.” 2 The. 2:3” 4, 7, Hata zamani zile aliona makosa yakiingia polepole kanisani» ambayo yangetengeneza njia ya kukuza utawala wa Kanisa la Kirumi.VK 16.1

  Polepole» kwa hila na kwa sin mwanzoni, ile siri ya kuasi iliendeleza kazi yake ya udanganyifu na kumtukana Mungu; lakini kwa kadiri ilivyozidisha nguvu na kuzitawala nia za watu, hivyo ndivyo alivyozidi kufanya kazi yake kwa wazi.VK 16.2

  Punde kwa punde, kwa kadiri isiyoonekana, madhehebu ya makafiri yaliingizwa katika kanisa la Kikristo. Kwa muda fulani ile nia ya kufanya mapatano na kuyaingiza madhehebu ya makafiri ndani ya kanisa ilizuiliwa kwa sababu ya mateso makali ambayo kanisa lilipata chini ya utawala wa ushenzi Lakini mateso yalipokoma, tena dini ya Kikristo ilipokaribishwa hata kwa majumba ya wafalme, kanisa lilianza kupjunguza hali yake ya kufafana na Kristo na mitume kwa unyenyekevu na unyofu, wakaanza kufanya fahari na kiburi sawa na mahaini na watawala wa dini ya kishenzi; na badala ya matakwa ya Mungu, kanisa liliweka mafundisho na maelezo ya kibinadamu. Kulikuwa na shangwe kuu Konstantine alipoongoka mnamo mwanzo wa karne ya nne baada ya Kristo; lakini kuongoka kwake kulikuwa kwa jina tu; ndipo mambo na matendo ya kidunia yakaingia kanisani» yakawa kama yakifunikwa na kuhalalishwa na haki ya kanisa. Halafu kazi ya uhalifu ikaendelea upesi. Dini ya ushenzi ijapokuwa ilionekana kana kwamba imeshindwa, ilikuwa ikishinda. Roho yake ndiyo iliyotawala kanisani. Madhehebu yake, kawaida zake na matendo yake ya sherehe, hata na mambo kama ya ushirikina yalichanganywa pamoja na imani na ibada ya wale wanaojidai kuwa ni wafuasi wa Kristo.VK 16.3

  Kwa ajili ya mapatano haya kati ya Ushenzi na Ukristo, aliadhimishwa yule mtu wa dhambi aliyetabiriwa kuwa ni mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya Mungu. Maungo makubwa haya ya dini ya uongo ndiyo kazi kubwa ya ajabu inayofanywa kwa nguvu ya Shetani,—inaonyesha kujitahidi kwake katika kujiweka katika kiti cha enzi, na kuitawala dunia jinsi apendavyo.VK 17.1

  Kwa vile kanisa lilivyotamani kupata faida na heshima ya kidunia, liliongozwa, kutaka fadhili na msaada kutoka kwa wakuu wa dunia; na kwa vile lilivyomkana Kristo, lilivutwa kujitia chini ya uongozi wa yule mwovu.VK 17.2

  Fundisho moja kuu la Kanisa la Kirumi ni ya kwamba papa (pope) ndiye kichwa kionekanacho cha Kanisa la Kristo katika mahali pote, ambaye amepewa utawala kabisa juu ya maaskofu na wahubiri wote duniani pote. Zaidi ya hayo, papa amejitwalia majina yale yanayokuwa ya Mungu hasa.VK 18.1

  Shetani alijua dhahiri ya kwamba kwa kusoma Maandiko Matakatifu wanadaniu wangeweza kufahamu madanganyifu yake na kuzuia nguvu zake. Hata Mwokozi wa ulimwengu alimpinga na Neno Takatifu. Kristo alimshinda kila mara akimpiga na ngao ya ukweli wa Mungu, kwa kusema, “Imeandikwa.” Alilipinga kila shauri la adui kwa hekima na uwezo wa Neno. Basi kama Shetani alitaka kudumu katika kuwatawala wanadamu na kuthibitisha mamlaka ya Kanisa la Kirumi, ambalo lilijitwalia nguvu isiyo yake, ilimpasa Shetani kuweka watu katika kutofahamu Maandiko Matakatifu. Biblia ingemtukuza Mungu na kuwafahamisha wanadamu hali yao ya kweli; na kwa hiyo ilikuwa ni lazima kuyafunga na kuyasetiri mafundisho matakatifu ya Biblia. Tena Kanisa la Kirumi likatumia njia hii. Kwa kame nyingi kuvieneza vitabu vya Biblia kulikuwa haramu. Watu walikatazwa wasiisome Biblia wala kuwa nayo nyumbani ; tena mapadre na maaskofu wapotovu wakaeleza mafundisho ya Biblia kwa namna ilivyoweza kuthibitisha uongo wao. Kwa njia hii papa alipata kukubaliwa karibu duniani pote ya kwamba yu kaimu wa Mungu duniani, ambaye amepewa mamlaka makuu juu ya kanisa na serikali pia.VK 18.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents