Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya Nne - Jinsi Luther Alivyoleta Matengenezo Makubwa

  *****

  KATI ya wale walioitwa kuliongoza kanisa kutoka katika giza ya mafundisho ya Kanisa la Kirumi wapate kuingia katika nuru na imani ya kweli, yule wa kwanza alikuwa Martin Luther. Alikuwa mwenye bidii na nguvu, mwenye kushika kazi kwa moyo, asiyemwogopa mtu ye yote ila Mungu tu, na asiyekubali msingi wo wote wa dini, isipokuwa Maandiko Matakatifu tu, Luther alikuwa mtu aliyefaa kabisa kuishi katika siku zile: Mungu alimtumia kwa kazi kubwa zaidi, yaani kazi ya kufanya matengenezo ya kanisa na kuleta mwanga katika dunia nzima.VK 35.1

  Siku moja, alikuwa akitazama vitabu katika chuo kikuu, Luther alipata Biblia ya Kilatini. Mpaka hapo alikuwa amesikia sehemu za Injili na Nyaraka zikisomwa katika mikutano ya ibada, akafikiri ya kwamba Neno la Mungu ndilo vitabu vile tu. Sasa alipata kuona Biblia nzima mara ya kwanza. Aliyafungua makaratasi ya Biblia kwa kicho, akastaajabu sana, alijisomea mwenyewe maneno ya uzima kwa haraka na moyo unaopigapiga, akitulia kidogo pengine, akisema, “Laiti Mungu anipe kitabu cha namna hiki kiwe changu mwenyewe!” Malaika za mbinguni walikuwa karibu naye, na nuru itokayo katika kiti cha enzi cha Mungu ilimfunulia mambo ya ajabu katika Biblia. Tangu zamani alikuwa akiogopa kumkosea Mungu, lakini wakati huo aliguswa zaidi moyoni akafahamu hali yake ya kuwa mwenye dhambi kwa namna asivyofahamu zamani. Alikuwa na hamu ya kuwekwa hum na dhambi na kufanya upatanisho na Mungu, na hali hiyo ilimwongoza hata akaingia katika nyumba ya watauwa akajitoa kuishi maisha ya utauwa pamoja na “monks” (ambao ni watu wajitengao na mambo ya dunia, ili wajifunge kwa mambo ya dini).VK 35.2

  Kila siku alipopata nafasi kidogo ya kupumzika, alitumia nafasi ile kwa kusoma, akijinyima usingizi, na pengine saa zake za chakula. Zaidi ya mambo yote alipenda kujifunza Neno la Mungu. Alipata Biblia ikifungwa na minyororo juu ya ukuta katika nyumba ile, na alijitahidi kuisoma mara kwa mara.VK 36.1

  Luther alitiliwa mikono kuwa kasisi, na akaitwa aondoke katika nyumba ile ya utauwa aishike kazi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Wittenbeg (yaani University). Hapo alianza kujifunza Maandiko Matakatifu katika lugha zilizoandikwa mwanzoni. Alianza kuwahutubia wanafunzi juu ya Biblia; na kitabu cha Zaburi, vitabu vya Injili, na Nyaraka zilifunuliwa na kuelezwa mbele ya makutano ya wasikilizaji waliopendezwa. Alikuwa hodari katika Maandiko Matakatifu, na neema ya Mungu ilimkalia. Ufasaha wa maneno yake uliwavuta sana wasikilizaji wake, akili timamu na uwezo wake wa kuuhubiri ukweli uliwasadikisha kabisa, na nguvu ya usemi wake iliwagusa mioyo.VK 36.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents