Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya Saba - Ujumbe Wa Malaika Wa Kwanza

    *****

    UNABII wa ujumbe wa malaika wa kwanza, ulioandikwa katika Ufunuo 14, ulitirnizwa katika miaka ya 1840-44, watu walipokuwa wakitazamia kurejea kwa Kristo. Katika nchi za Ulaya na Amerika, watu waliojaa imani na wenye bidii kwa kuomba walivutwa moyoni walipotazamishwa mambo yaliyotabiriwa, na kwa kuyachunguza sana Maandiko Matakatifu walipata maneno yaliyowasadikisha ya kwamba mwisho wa mambo yote ulikuwa umekaribia sana. Roho wa Mungu aliwavuta watenda kazi wa Mungu walitoe onyo lile kwa wengine. Po pote duniani ujumbe huu wa injili ya milele ulienea: “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.” Ufunuo 14:7.VK 53.1

    Po pote palipokwisha kuingiliwa na wamishenari, palitangazwa habari njema za kurudi kwa Kristo kulivyokaribia. Katoka nchi mbali mbali kulipatikana jamii za Wakristo ambao, kwa kuyachunguza sana Maandiko, walikuwa wamesadikishwa ya kwamba kurudi kwa Kristo kumekaribia. Katika nchi zingine za Ulaya, ambapo amri zilikuwa kali sana hata zikakataza kuhubiri habari za marejeo ya Yesu, watoto wadogo walitumiwa na Mungu ili waitangaze habari hiyo, na wengi wakasikiliza onyo lile.VK 53.2

    William Miller na watenda kazi wenzake ndio walipewa kazi ya kuuhubiri ujumbe huu katika Amerika, na mwanga uliotiwa na kazi zao ulimulika mpaka nchi za mbali. Mungu alimtuma malaika wake auamshe moyo wa mkulima fulani ambaye hakuyaamini mafundisho ya Biblia, apate kuongozwa kuyachunguza maneno ya unabii. Mtu yule maalum alijiwa na malaika mara kwa mara, kumwongoza na kumfungulia maneno ya unabii ambayo tangu zamani yalikuwa mafumbo kabisa kwa watu wa Mungu. Alipewa neno la kwanza katika mfululizo wa ukweli, naye aliongozwa kuendelea kutafuta hatua kwa hatua, mpaka alipopendezwa sana na kushangazwa na Neno la Mungu. Aliona ya kwamba ndani yake kulikuwa mwandamano kamili wa ukweli. Lile Neno la Mungu, ambalo mara ya kwanza alidhani ya kwamba halikuandikwa kwa maongozi ya Mungu, sasa aliweza kuona mwenyewe uzuri na utukufu wake. Aliona ya kwamba sehemu moja ya Maandiko hueleza maana ya sehemu nyingine, na asipoweza kufahamu sehemu fulani aliweza kupata maelezo yake katika sehemu nyingine ya Biblia. Alipendezwa sana na Neno la Mungu, tena aliona ya kwamba linafaa kuheshimiwa na kuangaliwa kwa kicho.VK 54.1

    Alipozidi kuchungulia mwandamano wa maneno ya unabii, aliona ya kwamba watu wakaao duniani wanaishi katika siku za mwisho kabisa ya mambo ya dunia hii, wala hawakujua. Aliyatazama makanisa, akaona ya kwamba yalipotoka, watu walikuwa wameacha kumpenda Yesu, wakaanza kuipenda dunia; walikuwa wakitafuta heshima na makuu ya dunia, badala ya kutaka heshima ile itokayo juu; walikuwa wanatamani mali za dunia, badala ya kuweka hazina zao mbinguni. Aliweza kuona unafiki, giza, na kifo kila mahali. Alichomwa sana moyoni. Mungu alimwita kusudi aliache shamba lake, jinsi alivyomwita Elisha awaache ng’ombe zake na kazi yake apate kumfuata Eliya.VK 54.2

    Kwa kicho na kutetemeka, William Miller akaanza kuwafunulia watu siri za ufalme wa Mungu, akiwafundisha wasikilizaji wake habari za unabii tangu zamani mpaka kufika wakati wa marejeo ya Kristo. Ushuhuda ulioandikwa katika Biblia uliowaongoza watu kufikiri ya kwamba Yesu atakuja katika mwaka wa 1843 uliwaamsha watu kila mahali. Wengi walisadiki ya kwamba maneno yaliyoelezwa juu ya nyakati za unabii yalikuwa sawa, na wakaacha kushika mashauri yao wenyewe, wakaupokea ukweli, kwa furaha. Wahubiri wengine waliacha fikara na maoni yao juu ya madhehebu ya dini, wakaacha mishahara yao, wakajiunga pamoja katika kutangaza habari ya kuja kwake Yesu.VK 55.1

    Walakini kulikuwa na wahubiri wachache tu, ambao walikuwa tayari kuukubali ujumbe huu; kwa hivyo kazi kubwa iliwekwa mikononi mwa washiriki wanyenyekevu. Wakulima waliyaacha mashamba yao, mafundi wa mashine waliziacha mashine zao, wafanyi biashara waliacha bidhaa zao, wataalamu waliacha shughuli zao; walakini watenda kazi walikuwa wachache sana wakilinganishwa na kazi iliyopasa kufanywa. Hali ya kutomcha Mungu ilivyokuwa Kanisani, na dunia jinsi ilivyo katika hali ya uovu, mambo haya yalilemea roho za watu wa Mungu wenye haki, hao nao walikuwa tayari kufanya kazi kwa nguvu, wakiivumilia dhiki na taabu, kusudi wapate kuwavuta watu waongoke moyo na kupata wokovu. Ingawa kazi ilipingwa sana na Shetani, lakini iliendelea mbele kwa nguvu, na ukweli wa marejeo ya Yesu ulikubaliwa na watu maelfu.VK 55.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents