Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ushindani

  Tangazo la wakati maalum wa kuja kwa Kristo lilileta ushindani mkubwa sana toka kwa watu wa kila aina, tangu wahubiri hata wenye dhambi wasiojali jambo lo lote, waliothubutu kumdharau Mungu. “Hakuna mtu ajuaye nyakati wala majira!” Maneno haya yalisikiwa yakisemwa na wahubiri wanafiki pamoja na wenye kudhihaki dini kabisa. Walikataa kuyasikia maelezo yaliyo dhahiri ya fungu hili yaliyotolewa na wale waliokuwa wakiwaonyesha jinsi mwisho wa nyakati zilizotabiriwa na manabii ulivyokaribia, pamoja na utumilizo wa ishara ambazo Kristo mwenyewe alikuwa amezitabiri ya kwamba zitaonyesha kuja kwake mara ya pili jinsi kulivyo karibu.VK 58.1

  Wengi wao waliokuwa wakijidai ya kwamba wanampenda Mwokozi wao, walisema ya kwamba hawana neno juu ya mahubiri ya kurejea kwake; lakini hawakukubali uwekwe wakati maalum wa kuja kwake. Mungu ajuaye yote alijua fikara za mioyo yao. Hawakupendezwa na jambo la kuja kwa Kristo ili kuihukumu dunia kwa haki. Walikuwa wametenda kama watumishi wasio waaminifu, matendo yao hayakustahili kukaguliwa na Mungu ajuaye fikara za mioyoni, hao nao waliogopa kumlaki Bwana wao. Hawakuwa tayari kumkaribisha Kristo kwa furaha, kama vile Wayahudi wasivyokuwa tayari kumpokea wakati wa kuja kwake mara ya kwanza. Shetani na malaika zake walisimanga wakamshutumu Yesu na malaika zake watakatifu, kwa kuwa watu wa Kristo walikuwa wakimpenda kidogo tu, wala hawakuwa na hamu ya kuonekana kwake.VK 58.2

  Walinzi wasio waaminifu waliyazuilia maendeleo ya kazi ya Mungu. Watu walipoamshwa mioyoni, na wakaanza kuitafuta sana njia ya wokovu, watangulizi hawa walijiingiza kati yao na ukweli, wakitaka kuutuliza woga wao kwa kueleza vibaya maana ya Neno la Mungu. Shetani na wahubiri wasiojitoa kweli kweli waliungana katika kazi hii na kusema, Amani, amani, ambapo Mungu hakusema neno lo lote juu ya amani. Wengine walikataa kuingia katika ufalme wa Mungu wao mwenyewe, na wale waliokuwa wakitaka kuingia waliwazuia, kama Mafarisayo walivyofanya katika siku za Kristo. Damu ya watu wale waliozuiliwa ufalme wa Mungu itatakiwa juu ya wale waliowazuia.VK 59.1

  Po pote ujumbe wa kweli ulipohubiriwa, ulikubaliwa mara ya kwanza na watu wanyenyekevu na waaminifu katika makanisa. Wale waliojisomea Biblia wenyewe, waliweza kutambua ya kwamba maelezo ya maneno ya unabii yaliyokubaliwa na wingi wa watu hayakupatana na maneno ya Biblia. Tena po pote ambapo watu hawakudanganywa na makasisi kwa vile walivyotoa maelezo ya uongo na kupotoa mambo ya dini, po pote walipokuwa wakichunguza Neno la Mungu wao wenyewe, ilitakiwa tu ili fundisho lile juu ya kurejea kwa Kristo lilinganishwe na Maandiko Matakatifu, ndipo lilithibitishwa kwamba ni jambo litokalo kwa Mungu.VK 59.2

  Watu wengi waliteswa na wenzao wasioamini. Kulikuwa na watu wengine, ambao kwa kutaka kudumu katika madarasa yao kanisani, walikubali kunyamaza wasiseme neno juu ya tumaini lao; lakini wengine waliona ya kwamba utiifu kwa Mungu ungewazuia wasiyafiche mambo ya kweli waliyokuwa wamekabidhiwa na Mungu. Watu wengi waliharimishwa kanisani kwa ajili ya sababu moja tu, yaani kuikiri imani waliyokuwa nayo juu ya kuja kwa Kristo. Maneno haya ya nabii yalikuwa na thamani kubwa kwa wale waliojaribiwa kwa. imani yao: “Ndugu zenu wawachukiao ninyi waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, na atukuzwe Bwana tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.” Isaya 66:5.VK 60.1

  Malaika za Mungu walichungulia kwa makini sana matokeo ya onyo lile. Wakati ambapo makanisa yalikataa ujumbe, malaika wakawaacha kwa huzuni. Walakini, kulikuwako na wengi katika makanisa ambao walikuwa hawa-jajaribiwa bado juu ya ukweli ule wa marejeo ya Kristo. Wengi walidanganywa na waume wao, wake zao, wazazi wao au watoto wao, wakasadikishwa ya kwamba ni dhambi hata kuyasikiliza maneno yale ya uzushi yaliyofundishwa na Waadventista, yaani wale waliotazamia kurudi kwa Kristo. Malaika waliambiwa wawalinde watu hawa vizuri; kwa kuwa mwanga mwingine ulikuwa ukiwajia kutoka katika klti cha enzi cha Mungu.VK 60.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents