Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kukawia! Kukawia!

  Ndipo nikamwona Yesu akiyavua mavazi yake ya ukuhani, akajivika mavazi ya kifalme kabisa. Kichwani mwake zilikuwako taji nyingi, taji moja juu ya taji nyingine. Alitoka mbinguni akizungukwa na jeshi la malaika. Mapigo yalikuwa yakiwaangukia watu duniani. Wengine walikuwa wakimkana Mungu na kumlaani. Wengine walienda upesi kwa watu wa Mungu, wakiwasihi wawaonyeshe jinsi wanavyoweza kuziepuka hukumu zake. Lakini watakatifu hawakuwa na msaada wo wote wa kuwapa. Hakuna machozi tena kwa ajili ya wenye dhambi, walikuwa wameombewa mara ya mwisho, mzigo wa mwisho ulikuwa umechukuliwa kwa ajili yao, na onyo la mwisho lilikuwa limekwisha kutolewa. Hakuna sauti ya rehema ilivoweza kuwaita tena, wakati ambapo watakatifu na jeshi zima la mbinguni walikuwa wakijishughulisha na wokovu wao, wao wenyewe hawakujishughulisha kamwe ili wapate kuokoka. Uzima na mauti yalikuwa vamewekwa mbele yao kusudi wachague. Wengine walikuwa na hamu ya kuupata uzima, lakini hawakujitahidi kuupata. Hawakuchagua uzima, na sasa damu haikupatikana ya kuwatakasa wenye hatia hakuna tena Mwokozi mwenye rehema atakayewaoinbea akisema, ‘‘Waachie, waachie wenye dhambi muda kitambo tena.” Jeshi zima la mbinguni liliungana na Yesu walipoyasikia maneno haya, “Imetimia. Imekwisha.” Azimio la wokovu lilikuwa limetimia, lakini wachache tu waliochagua kuupokea wokovu ule. Na sauti nzuri ya rehema ilipofifia, waovu wakashikwa na woga na hofu kuu. Walisikia maneno haya yakisemwa kwa udhahiri sana, “Mmekawia! mmekawia ajabu!”VK 111.1

  Wale ambao hawakulithamini Neno la Mungu walikuwa wakienda hima huko na huko, wakizungukazunguka toka nchi fulani mpaka nchi nyingine, na kutoka magha ribi mpaka mashariki, wakilitafuta Neno la Mungu. Malaika akasema, “Hawatalipata Neno la Mungu wanaln tafuta. Kuna njaa kuu duniani; wala si njaa ya chakula, wala kiu ya maji, bali ni njaa na kiu ya kuyasikia maneno ya Mungu. Wangekubali kutoa cho chote ili wapate kusikia neno lo lote la sifa kutoka kwa Mungu! lakini hapana; ni lazima waendelee kuisikia njaa na kiu. Siku kwa siku walikuwa wakidharau wokovu, wakihesabu mali na anasa za dunia kuwa ya thamani kuu zaidi ya hazina na vitu vya kutamanisha vilivyo mbinguni. Wamemkataa Yesu na kuwadharau watakatifu wake. Inawapasa wachafu kuendelea kuwa wachafu milele.”VK 112.1

  Wingi wa waovu walikasirika sana walipoyasikia maumivu ya yale mapigo. Ulikuwa wakati wa maumivu makuu. Wazazi walikuwa wakiwalaumu watoto wao kwa ukali, na watoto kadhalika wakiwalaumu wazazi wao, tena ndugu na dada wakawa wakilaumiana. Vilio vya maombolezo vilisikika kila upande, wakisema, “wewe ndiwe uliyenizuia nisipate ukweli huu ambao ungeniokoa katika wakati huu wa hatari.” Watu waliwageukia wahubiri wao wakiwachukia na kuwalaumu wakisema, “Ninyi hamkutuonya. Mlituambia ya kwamba watu wote wataongoka, mkapaaza sauti zenu mkisema, Amani, amani, kusudi mwitulize hofu yote tuliyokuwa nayo. Hamkutuambia juu ya wakati huu; na wale waliokuwa wakituonya juu ya wakati huu, mliwaita wazushi na waovu waletao dini za uongo, zilizoweza kutuangamiza.” Lakini naliona ya kwamba wahubiri hawakuepukana na ghadhabu ya Mungu. Maumivu yao yalizidishwa mara kumi ya yale ya watu wao.VK 113.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents