Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya Ishirini Na Tatu - Mauti Ya Pili

  *****

  SHETANI atashangazwa sana akiiona fahari na utukufu wa Kristo. Yeye ambaye mara ya kwanza alikuwa kerubi mwenye kusitiri, atakumbuka siku ya kuanguka kwake. Yule ambaye alikuwa serafi anayeng’aa, “mwana wa asubuhi,” amebadilika, naye ameshushwa ajabu!VK 136.1

  Shetani ataona ya kwamba uasi wake aliouanzisha mwenyewe umemfanya asiwe na haki ya kuingia mbinguni. Daima amekuwa akizoeza nguvu zake kwa kushindana na Mungu, na kwa hivyo utakatifu, amani na usikilizano wa mbinguni ungekuwa kwake kama maumivu makali sana. Mashtaka yake yote juu ya rehema na haki za Mungu yatakomeshwa. Lawama zote alizokuwa akiweka juu ya Mungu, zitawekwa juu yake mwenyewe. Ndipo Shetani atainama na kuungama haki ya adhabu yake.VK 136.2

  Mambo yote ya ukweli na ya uongo katika shindano ambalo limeendelea tangu miaka mingi yatadhihirishwa. Haki na uadilifu wa Mungu vitadhihirishwa na kuthibitishwa kabisa. Walimwengu wote wataona jinsi Baba na Mwana walivyokuwa wamejinyima ajabu kwa ajili ya wanadamu. Wakati utakuwa umefika kwa Kristo kuketi juu ya kiti cha enzi kwa kuwa anastahili, naye atatukuzwa zaidi ya falme na mamlaka zote. na jina lake litatukuzwa zaidi ya majina yote.VK 136.3

  Ingawa Shetani atashurutishwa kukiri ya kwamba hukumu zaMungu ni za haki, na kufanywa kujiinamisha mbele ya mamlaka na utukufu wa Kristo, lakini tabia zake zitadumu kuwa zile zile za zamani, wala hazitageuzwa. Moyo wa uasi utaonekana kwake ukiamshwa tena kwa nguvu kama nguvu ya tufani. Kwa moyo wa ghadhabu ataikaza nia yake asije kushindwa katika lile shindano kuu. Wakati wake utafika wa kufanya mashindano makali zaidi juu ya Mfalme wa mbinguni. Ndipo ataingia kati ya watu wake, atajaribu kuwafanya wawe na ghadhabu kama yake, na kuwachochea waanze kupiga vita mara. Lakini kati ya watu mamilioni ambao amewadanganya ili wamwasi Mungu, hakuna hata mmoja atakayckubali mamlaka yake. Uwezo wake wote utakoma. Waovu watajaa ile chuki inayomshika Shetani; lakini wataona ya kwamba hawawezi kitu, kwa kuwa hawawezi kumshinda Mungu. Ghadhabu yao itaanza kuwaka juu ya Shetani na wale waliomsaidia katika kazi ya udanganyifu. Watawarukia kwa uwezo mkuu kama wa mashetani, ndipo vita vitakuwa ulimwenguni pote.VK 137.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents