Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Siku za Taabu

  Siku zile zilikuwa siku za taabu kwa kanisa la Kristo. Watu waliokuwa thabiti kweli kweli walikuwa wachache sana. Ingawa mashahidi wengine walibaki ili kuutunza ukweli, lakini mara zingineilionekana ya kwamba dhambi na ibada ya namna ya ushirikina llikaribia kushinda, na dini ya kweli ilikuwa karibu kutoweka kabisa duniani. Injili ilisahauliwa, lakini mifano mitupu ya dini ilizidishwa, na watu walilemewa kwa kutozwa fedha nyingi isiyo ya haki.VK 24.3

  Si kwamba walifundishwa tu kumtazamia papa kuwa mpatanishi wao, lakini pia walifundishwa wapate kuzitegemea kazi zao wenyewe kusudi waupate upatanisho wa dhambi. Safari ndefu. adhabu za makosai, kuyaabudu makumbusho ya watakatifu wa kale, kuyajenga makanisa, mahali pa sanamu, na madhabahu, na kulipa pesa nyingi kwa kanisa—haya yote na matendo mengine’ ya namna hayo yalishurutishwa kwa nguvu makusudi kuituliza ghadhabu ya Mungu, au wapate kufadhiliwa na Mungu; kana kwamba Mungu, hufanana na wanadamu, tena hasira yake huwaka kwa mambo ya upuzi, au anaweza kutulizwa na sadaka au vitubio!VK 25.1

  Kame nyingi zilipoongezeka, ikaonekana ya kwamba makosa ya mafundisho yaliyotolcwa na Rumi yalikuwa yakiongezeka sana. Hata kabla ya kuimarishwa kwa mamlaka ya Papa, mafundisho ya washenzi wenye elimu yalikuwa yameingia kanisani. Wengi ambao walijidai ya kwamba wameongoka moyo, walikuwa wakiyashikilia madhehebu ya elimu ya kishenzi, tena hawakuendelea kujifunza mambo yao peke yao tu, bali waliwashurutisha wengine kuyapokea mafundisho yale, ili kwa njia ile wapate kuwa na nguvu na mvuto miangoni mwa wasfienzi. Hivi mafundisho makubwa ya uongo yalianza kuingia katika dini ya Kikristo. Mojawapo lililo kuu zaidi kati ya haya lilikuwa fundisho lililosema ya kwamba wanadamu wana hali ya kuishi milele, na ya kwamba wafu huwg na ufahamu wa nafsini. Fundisho hili la uongo ndilo lililokuwa asili ya kawaida ya Kirumi ya kuwaabudu watakatifu wa zamani na kumsujudu Mariamu. Tokea fundisho hili, uzushi mwingine ukatokea ya kwamba wale wasiogeuka mwishoni, watateketezwa milele; fundisho hili lilipokewa na kuwa kanuni ya dini ya Kirumi wakati uasi ulipokuwa umeanzishwa karibuni.VK 25.2

  Ndipo njia ikatengenezwa tena kwa uvumbuzi wa namna nyingine ya ushenzi, ambao Warumi waliuita “Purgatory”, (yaani mahali pa kuwatakasa watu waliokufa); na njia hiyo ikatumiwa kwa kuwaogofisha watu wengi waliokuwa wajinga na washirikina. Uzushi huu ndio unaosema ya kwamba pana mahali pa ahera pa maumivu makali, ambapo watu wasiostahili kuhukumiwa milele wataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao, na baadaye wakisha kutakaswa na unajisi wao, ndipo watakapokubaliwa kuingia mbinguni.VK 26.1

  Lakini fundisho jingine lilikuwa lazima kubuniwa, kusudi kuiwezesha Rumi kujifaidia na hofu na makosa ya wafuasi wake. Likabuniwa fundisho juu ya jambo liitwalo “ Indulgence,” yaani ahadi ya kuachiliwa dhambi, kwa ajili ya kufanya jambo fulani. Maondoleo kabisa ya dhambi, yaani dhambi zilizopita, za sasa na zitakazofanywa baadaye, na kuondolewa maumivu yote na adhabu zote zipasazo, mambo hayo yote yaliahidiwa kwa wale waliokubali kujitoa kwa kupiga vita vya papa kwa kuieneza milki yake ya dunia hii, kuwatesa adui zake, au kuwaharibu wale waliothubutu kuukanusha ukuu wake. Watu walifundishwa pia ya kwamba kwa kulipa pesa kwa kanisa, waliweza kuondolewa dhambi, na pia kuwaweka huru rafiki zao waliokuwa wakiadhibika katika ndimi za moto. Hii ndiyo njia ambayo kwayo Rumi ilijaza masanduku yake ya pesa, na kuufululiza utajiri, fahari, na ufisadi wa wale waliojidai kuwa wajumbe wa Yule asiyekuwa na mahali pa kulaza kichwa chake.VK 26.2

  Agizo la Biblia juu ya meza ya Bwana lilikuwa limeondolewa, na badala yake iliwekwa ibada ya Misa, ambayo ni kama ibada ya sanamu. Kwa njia ya kufanya mambo yasiyo na maana, makasisi wa Kanisa la Kirumi walijidai ya kwamba walikuwa na uwezo wa kugeuza mkate na mvinyo kuwa mwili na damu ya Kristo kweli. Kwa ufidhuli na makufuru walijidai ya kwamba wana uwezo wa “Kumwumba Muumba wao.’’ Wakristo wote walishurutishwa kukiri kwamba waliamini uzushi huu ambao kweli ulikuwa ukimtukana Mungu ama wapate adhabu ya kufa. Wale waliokataa kuufuata uzushi huo waliteketezwa kwa moto.VK 27.1

  Mamlaka ya Rumi yalipozidi kuenea, ndipo uovu wao ukaongezeka duniani. Maandiko Matakatifu yalikaribia kupotea kabisa, si kwa watu peke yao, bali na kwa makasisi pia. Kama Mafarisayo wa zamani, watangulizi wa Kirumi waliuchukia mwanga, usije ukazifunua dhambi zao. Baada ya kuiondoa sheria ya Mungu, ambayo ilikuwa kipeo cha ukamilifu, wakaanza kutumia nguvu bila kiasi, wakatenda mabaya bila kizuizi. Ulaghai, tam’aa ya mali; na uasherati ukazidi. Watu hawakuepukana na tendo lo lote la uhalifu lililoweza kuwaletea mali au cheo. Majumba ya mapapa na maaskofu yalijaa zinaa na ulevi. Mapapa wengine wakuu walifanya mambo ya uhalifu na kuchukiza mno, hata watawala wa serikali ya nchi walijaribu kuwauzulisha wale wakuu wa kanisa, wakiwaona kuwa ni watu wabaya kabisa wasiostahili kuyashika madaraka ya heshima. Kwa kame nyingi hayakuwa na maendeleo yo yote kwa kuelimisha watu, kwa kazi ya ustadi, wala kwa ustaaarabu. Mambo ya kiroho na ya elimu yalizimishwa kabisa katika nchi zote za Kikristo. *Maana ya maneno yaliyoandikwa katika Kilatini katika ukurasa 19: Constantino, mfalme August, kwa Helpidius: Katika siku kuu ya jua (Jumapili) madiwani wote na watu wote wakaao katika miji na wapumzike, tena viwanda vyote vya kazi vifungwe. Lakini katika vijiji, watu wanaofanya kazi ya ukulima, sheria inawaruhusu kuendelea kufanya kazi zao: kwani pengine inaonckana ya kwamba siku hiyo inafaa sana kwa kupanda mbegu za miche ya mizabibu kuliko siku nyingine: kwani wasipofanya hivyo, labda siku zinaweza kuwapitia ambazo zinafaa Sana kwa kazi hizo kuliko siku zingine, tena wakikosa kupanda, mibaraka ya mbinguni inaweza kuwapitia. (Maneno haya yametolewa katika: Schaff’s History of the Christian Church, Vol. Ill, section 75, paragraph 5. Note 1).VK 27.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents