Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kujitayarisha Kumlaki Bwana

  Wale waliokuwa wameupokea ujumbe ule walikesha kwa hamu kubwa sana wakitazamia kuja kwa Mwokozi wao. Wakati ambapo walikuwa wakitazamia kumlaki Bwana uliwadia. Waliutazamia wakati ule kwa kicho na unyofu wa moyo. Walistareheka katika kuzungumza na Mungu, wakiitazamia amani kuu waliotumaini kupata baadaye katika ufalme wake. Hakuna mtu ye yote kati ya wale walioshiriki tumaini na imani ile aliyeweza kuzisahau nyakati zile za kumngoja Bwana. Shughuli za kawaida za kidunia ziliachwa kwa majuma kadha. Waaminio walijiangalia sana fikara na nia zao kana kwamba walitaka kufa, na ya kwamba baada ya muda kitambo macho yao yatafumbwa wasiyatazame mambo ya dunia tena. Hawakuzitengeneza kanzu za kupaa mbinguni, (kama wengine wasemavyo), lakini wote walikuwa na hamu ya kuthibitisha moyoni ya kwamba walikuwa tayari kumlaki Mwokozi wao, mavazi yao meupe ndiyo usafi wa moyo, tabia iliyotakaswa na dhambi kwa damu ya upatanishi wa Kristo.VK 61.1

  Mungu alikusudia kuwajaribu watu wake. Mkono wake ulilifunika kosa fulani katika kuzihesabu nyakati zilizotabiriwa. Wale watu waliokuwa wakimtazamia Bwana hawakulitambua lile kosa, wala adui zao walioelimika sana hawakulitambua. Adui zao walisema hivi: “Hamkukosa hata kidogo katika kuzihesabu nyakati za unabii. Kuna jambo kubwa fulani litakalotokea baada ya siku si nyingi. lakini si jambo lile ambalo William Miller analitabiri; jambo hilo ndilo kuongoka kwa walimwengu wote. wala si kuja kwa Kristo mara ya pili.”VK 61.2

  Wakati ule wa kumngoja Bwana ulipita, na Kristo hakuonekana kwa kuwaokoa watu wake. Wale ambao walimngojea Mwokozi wao kwa imani na upendo mkuu waiiona uchungu mkuu sana. Walakini Bwana alikuwa amelitimiza kusudi lake: alikuwa amejaribu mioyo ya wale waliojidai ya kwamba walitazamia marejeo yake. Miongoni mwao kulikuwa na wengine ambao walivutwa na woga tu, wala hawakuwa na moyo hasa wa kumtazamia. Ungamo la tumaini )ao halikugeuza hali ya mioyo yao wala maisha yao. Tokeo lile kuu lililotazamiwa lilipokosa kutimia, ndipo watu hawa wakasema ya kwamba hawana uchungu moyoni; kwani hawakuamini ya kwamba Kristo atakuja. Wao ndio waliokuwa kati ya watu wa kwanza waliochekelea huzuni ya waaminio wa haki.VK 61.3

  Lakini Yesu na malaika wote wa mbinguni waliwaangalia kwa upendo na rehema wale ambao, ingawa walijaribiwa na kuhuzunishwa, walidumu kuwa waaminifu. Kama kitu kinachotenga mambo yanayoonekana na yasiyoonekana kingaliweza kuondolewa ndipo malaika wangalionekana wakiwakaribia wale waliokuwa waaminifu, wakiwalinda na mishale ya madanganyifu ya Shetani.VK 62.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents