Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya Tano - Maendeleo Ya Matengenezo Ya Dini

  *****

  MFALME mwingine, aitwaye Charles wa Tano, alifanywa mfalme wa Ugermani. na wajumbe wa Rumi walienda upesi kumpelekea barua za jifa, wakitaka kumshawishi yule mfalme atumie uwezo wake kwa kushindana na wale waongozi wa Matengenezo ya dini. Lakini liwali mmoja, Elector wa Saxony, ambaye alimsaidia Charles kuwekwa kuwa mfalme, alishauri asifanye jambo lo lote la kumdhuru Luther mpaka atakapomwita katika baraza.VK 42.1

  Jamia za watu wa Udachi walitazamia baraza kuu la majimbo yote iliyokuwa karibu kukutanika katika mji wa Worms muda kitambo baada ya kutawazwa kwa Charles kuwa mfalme. Kulikuwa na mambo makuu yaliyohusika na utawala wa nchi, ambayo yalipaswa kufikiriwa na baraza hii kuu ya nchi; lakini mambo haya yote yalionekana kwamba hayana maana sana yakilinganishwa na kazi ya yule mtauwa shujaa wa Wittenberg.VK 42.2

  Mara ya kwanza Charles alikuwa amemwambia yule elector wa Saxony amlete Luther katika ile Baraza kuu, akimhakikishia ya kwamba Luther atalindwa na matendo yote ya jeuri, na ya kwamba atakubaliwa kupewa mtaalamu fulani awezaye kujadiliana naye juu ya mambo makuu hasa yaliyoleta mabishano. Luther mwenyewe alikuwa na hamu ya kuonekana mbele ya mfalme.VK 42.3

  Rafiki za Luther waliogopa na kushangaa. Kwa jinsi walivyojua chuki na uadui wa watu wale juu yake Luther, waliogopa ya kwamba isingeheshimiwa ile hati ya kusafiri salama, na walimshauri ili asijihatarishe maisha yake. Alijibu hivi: “Wajumbe wa Papa hawataki nifike Worms, lakini wanataka nihukumiwe na kuuawa. Lakini haidhuru. Msiniombee mimi, bali liombeeni Neno la Mungu.”VK 43.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents