Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Moto Kutoka Mbinguni

  Ndipo maneno haya ya unabii yatakapotimia: “Maana Bwana ana ghadhabu juu ya mataifa yote. na hasira kali juu ya jeshi lao lote: amewaangamiza kabisa, amewatoa waende kuchinjwa.” Isaya 34:2. “Awanyeshee wasio haki mitego; moto na kiberiti, upepo wa hari, na viwe fungu la kikombe chao.” Zaburi 11:6. Moto utashuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Dunia itavunjika kabisa. Silaha ambazo zimefichika chini ya ardhi zitaondolewa. Moto uteketezao utatoka katika kila shimo. Hata miamba itawaka moto. Siku itakuwa imekuja ambayo “inawaka kama tanuru.” Malaki 4:1. “Viumbe vya asili vitaunguzwa na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.” (2 Petro 3:10). Moto wa Tofeth umewekwa kwa mfalme wa uasi, ameifanya kubwa, inakwenda chini sana; tanuru yake ni moto na kuni nyingi: na “pumzi ya Bwana, kama moto wa kiberiti, huiwasha.” Isaya 30:33. Uso wa dunia utaonekana kama kitu kilichoyeyushwa—kama ziwa kuu la moto. Hii ndiyo siku ya hukumu na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu—“siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni.” Isaya 34:8.VK 137.2

  Waovu watapata ijara yao duniani. “Watakuwa makapi: na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi.” Malaki 4:1. Wengine wataharibiwa mara moja lakini wengine wataendelea kupata maumivu kwa siku nyingi. Wote wataadhibiwa kwa namna ya matendo yao. Dhambi zote za watakatifu zitawekwa juu ya Shetani, mwanzishaji wa uovu, yeye ndiye atakayechukua adhabu yao. Hivyo ataadhibiwa, si kwa ajili ya uasi wake peke yake, lakini pia kwa ajili ya dhambi zote ambazo aliwafanya watu wa Mungu kuzitenda. Adhabu yake itakuwa kali mno zaidi ya wale ambao aliwadanganya. Baada ya wote waliodanganywa naye kufa wote, yeye ataendelea kuishi akiumizwa kwa muda fulani. Katika moto wa mwisho wa kuitakasa dunia, waovu wote wataharibiwa, shina na tawi —Shetani ndiye shina, na wafuasi wake ndio matawi. Haki ya Mungu itaridhika, na watakatifu na jeshi lote la malaika watasema kwa sauti kuu, Amina!VK 138.1

  Dunia itakapokuwa ikiteketea kwa ghadhabu ya Mungu, watakatifu watakaa salama katika Mji Mtakatifu. Mauti ya pili haitakuwa na nguvu juu yao walio na sehemu katika ufufuo wa kwanza. (Ufunuo 20:6). Kwao waovu Mungu atakuwa moto ulao, lakini kwa watakatifu wake atakuwa jua na ngao. (Zaburi 85:11).VK 139.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents