Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuenea kwa Matengenezo

    Kwa ajili ya maandiko ya Wycliffe, John Huss, mwenyeji wa Bohemia, alikata shauri kuyakataa mafundisho ya Kirumi, yasiyo ya kweli akajiunga katika kazi ya matengenezo. Huss pia alikuwa Mkristo mashuhuri kama Wycliffe, tena alikuwa mtu aliyeelimika sana, na mwenye nia ya kujitoa kwa ukweli wa Mungu bila kurudi nyuma. Watu wengi waliamshwa movo na mafundisho yake yaliyoshikamana na Biblia, na kwa jinsi alivyowashitaki makasisi juu ya maisha yao ya kuchukiza na ya ufisadi, na watu maelfu wakafurahi kuyafuata yale mafundisho mapya yaliyokuwa safi na yenye haki. Jambo hili liliwaghadhabisha sana Papa na maaskofu, makasisi na watauwa (monks), tena Huss aliitwa mbele ya Baraza Kuu ya Constance (Council of Constance) apate kuhukumiwa kwa ajili ya uzushi. Alipewa hati ya kusafiri salama na mfalme wa Ugermani, na alipohka katika mji wa Constance aliahidiwa na Papa mwenyewe ya kwamba hatadhulumiwa katika hukumu.VK 32.1

    Baada ya kesi yake kusikizwa kwa siku nyingi, naye akishikilia ukweli, Huss aliambiwa achague kuvakana mafundisho yake au kuuawa. Alichagua kufa kama shahidi wa Mungu, na alipokwisha kuona vitabu vyake vikifeketezwa katika moto, yeye naye akaunguzwa pale pale. Mbele ya wakuu wa kanisa na serikali, mtumishi wa Mungu alikanusha kabisa machafuko ya utawala wa makasisi. Kuuawa kwake kinyume cha ahadi kuu iliyotolewa kwake kwa wazi mbele ya watu wote, ya kama atalindwa salama, kuliwadhihirishia walimwengu wote ukatili na uhaini wa Rumi. Wale adui za ukweli, ingawa hawakujua hivyo, kwa kweli walikuwa wakiendesha mbele kazi ya Mungu ambayo walijaribu kuiharibu wasifaulu.VK 32.2

    Ijapokuwa mateso yaliendelea vikali, walikuwako watu ambao kwa upole, kwa bidii, na kwa ustahimilivu waliendelea kuudakuliza uovu na upotovu wa mafundisho ya dini, hata baada ya kufa kwa Wycliffe. Watu wengi walitoa mali zao za kidunia kwa kuiendesha kazi ya Kristo kama ilivyokuwa katika siku za mitume.VK 33.1

    Jitahidi nyingi sana zilifanywa ili kuongeza nguvu na kuieneza mamlaka ya Kanisa la Kirumi, lakini ingawa maaskofu wakuu waliendelea kujidai ya kwamba ni wajumbe wa Kristo, maisha yao yalikuwa mabaya hata kuwachukiza watu. Kwa ajili ya uvumbuzi wa mtambo wa kupiga chapa, Maandiko Matakatifu yalizidi kuenea mahali pengi, na watu wengi walianza kuona ya kwamba mafundisho ya Kanisa la Kirumi hayakutegemezwa na Neno la Mungu.VK 33.2

    Shahidi mmoja alipozimishwa ndipo mwingine aliposimama na kwa ushujaa mkuu akaitangaza kweli. Vita vilianzishwa ambavyo matokeo yake yalikuwa uhuru, si wa watu mmoja mmoja, au kwa makanisa tu, bali uhuru wa mataifa. Ilikuwa kama watu walinvosha mikono yao kuishika ile kweli ya wale waaminifu wa siku za Wycliffe zamani ya miaka mia moja. Martin Luther alianzisha Matengenezo ya Kanisa katika Ugermani: Calvin alikuwa akiihubiri injili katika Ufransa, na Zwingle alikuwa akihubiri katika Switzerland. Dunia iliamshwa kutoka katika usingizi wa kiroho uliokuwa ukiishika tangu karne nyingi, na katika kila nchi maneno haya yalisikika, “Uhuru wa kila mtu kuabudu apendavyo.”VK 33.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents