Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kilio kwa Kupata Kuokolewa

  Wakati ule ulikuwa wakati wa maumivu makuu ya rohoni kwa watakatifu. Walimlilia Mungu nichana na usiku apate kuwaokoa. Kwa kadiri ilivyoonekana, haikuwezekana kwao kuokolewa. Waovu walikuwa wameanza kushangilia tayari, wakisema kwa sauti kuu, “Mbona Mungu wenu hawaokoi ninyi katika mikono yetu? Kwa nini hampandi juu mkayaokoe maisha yenu?” Lakini watakatifu hawakuwasikiliza. Walijitahidi katika kumwomba Mungu kama Yakobo alivyofanya. Malaika walikuwa na hamu ya kuwasaidia, lakini iliwapasa kungoja kidogo; ni lazima watu wa Mungu wanywe katika kikombe kile, na kubatizwa na ubatizo ule. Malaika, kwa jinsi walivyokuwa waaminifu kwa kazi yao, waliendelea kungoja. Mungu asingeacha jina lake lilaumiwe na washenzi. Wakati ulikuwa umewadia ambapo ilimpasa kuuonyesha uwezo wake na kuwaokoa watakatifu wake kwa utukufu. Kwa ajili ya utukufu wa jina lake angewaokoa wote ambao walingoja wakimtazamia, na ambao majina yao yameandikwa katika kitabu. Nalionyeshwa mzee Nuhu aliyekuwa mwaminifu. Mvua jliponyesha na Gharika ilipokuja, Nuhu na jamaa zake walikuwa wameingia katika safina, na Mungu alikuwa amewaonya watu walioishi kabla ya gharika lakini walimdharau na kumcheka tu. Tena maji yaliposhuka duniani, na watu wakaanza kuzama mmoja mmoja, waliiona safina ile, waliyoichezea na kuifanyia mzaha, ikielea salama juu ya maji, ikiwaokoa Nuhu mwaminifu na watu wa nyumba yake. Kadhalika naliona ya kwamba w atu wa Mungu, ambao kwa uaminifu waliwaonya watu wa dunia juu ya ghadhabu ya Mungu ijayo, wataokolewa. Mungu hatawaacha waovu wawaharibu wale wanaotazamia kuhamishwa duniani, na ambao walikataa kumsujudu mnyama na kuipokea alama yake. Naliona ya kwamba kama waovu wangeruhusiwa kuwaua watakatifu, ndipo Shetani na jeshi lake pamoja na wote wanaomchukia Mungu wangependezwa. Shetani angeshangilia ajabu kama katika vita vya mwisho angeweza kushinda wale ambao kwa muda mrefu wamemngoja Yule wanayempenda! Wale ambao wameidharau hali ya kupanda kwa watakatifu wa mbinguni, wataona utunzaji wa Mungu kwa watu wake, na wataona wokovu wao wa ajabu.VK 115.2

  Watakatifu walipotoka katika miji na vijiji walikimbizwa na waovu, wakitaka kuwaua. Lakini panga zilizoinuliwa kwa kuwaua watu wa Mungu zilivunjika zikawa hazina nguvu kama nyasi. Malaika za Mungu waliwalinda watakatifu. Walipomlilia Mungu mchana na usiku, kilio chao kilifika mbele za Mungu.VK 116.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents