Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Unabii juu ya Eliya, Sura ya 14

    Angalieni nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana. Malaki 4:5, 6.Mar 22.1

    Wale watakaoandaa njia kwa ajili ya kuja kwa Yesu mara ya pili, wanawakilishwa na Eliya aliyekuwa mwaminifu, kama vile Yohana alivyokuja katika roho ya Eliya kuiandaa njia kwa ajili ya ujio wa kwanza wa Kristo.Mar 22.2

    Kazi ya Yohana Mbatizaji na ile ya wale ambao katika siku za mwisho watakwenda katika roho na nguvu ya Eliya kuwaamsha watu kutoka katika kutokujali kwao, zinafanana katika mambo mengi. Kazi ya Yohana ni kielelezo cha kazi ambayo inapasa kufanywa katika kizazi hiki. Yesu anakuja mara ya pili kuuhukumu ulimwengu katika haki.Mar 22.3

    Yohana alijitenga na marafiki zake na akajitenga na starehe za maisha. Usahili wa mavazi yake, vazi lililofumwa kwa singa za ngamia, ulikuwa kemeo la kudumu dhidi ya ufujaji na kujionesha kwa makuhani wa Kiyahudi, pamoja na watu kwa ujumla. Mlo wake wa mboga, nzige na asali ya mwituni, ulikuwa kemeo dhidi ya uendekezaji wa tamaa na ulafi uliokuwa umeshamiri kila mahali. ... Somo kuu la matengenezo linapaswa lisisitizwe na mioyo ya watu iamshwe. Kiasi katika mambo yote inabidi kiunganishwe na ujumbe, kuwageuza watu wa Mungu kutoka katika ibada ya sanamu, ulafi, na ufujaji katika mavazi na mambo mengine.Mar 22.4

    Kujikana nafsi, unyenyekevu na kiasi vinavyotakiwa miongoni mwa wenye haki, ambao Mungu anawaongoza kwa namna ya pekee na kuwabariki, vitawakilishwa kwa watu kinyume na tabia za ufujaji zinazoathiri afya za wale wanaoishi katika kizazi hiki kilichoharibika. Mungu ameonesha kuwa matengenezo ya afya yanahusiana moja kwa moja na ujumbe wa yule malaika wa tatu kama vile mkono unavyohusiana na mwili.Mar 22.5

    Kama vile Yohana Mbatizaji... alivyowakumbusha Amri Kumi, ndivyo tunavyopaswa kuutoa ujumbe kwa sauti isiyo na mashaka: “Mcheni Mungu na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.” Tunapaswa kujitahidi kuiandaa njia ya kuja kwa Kristo mara ya pili kwa umakini uliokuwa kwa Eliya na Yohana Mbatizaji.Mar 22.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents