Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Je, Unao Ujasiri wa Kuwa Tofauti?, Sura ya 43

    Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu. 1 Petro 2:9.Mar 51.1

    Onyo litolewalo kuwa Mwana wa Adamu anakaribia kuja katika mawingu ya mbinguni Umekuwa kwa wengi kama kisa cha kawaida. Wameacha mkao wa kukesha na kungoja. Roho ya ubinafsi, na ya kidunia inayodhihirishwa katika maisha inafunua hisia zilizomo mioyoni, kama yule mtumwa aliyesema, “Bwana wangu anakawia kuja.”. . .Mar 51.2

    Roho ile ile ya ubinafsi, ya kukubaliana na mazoea ya kidunia, inaendelea katika siku zetu kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu. Wengi wanaodai kuwa watoto wa Mungu wanafuata matashi ya ulimwengu kwa nguvu inayoonesha walivyo waongo katika kujiita kwao watoto wa Mungu. Watakuwa wakipanda na kujenga, wakinunua na kuuza, wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, hadi wakati wa mwisho kabisa wa rehema yao. Hii ndiyo hali halisi ya walio wengi kati ya watu wetu. . .Mar 51.3

    Roho yangu inalemewa ionapo upungufu mkubwa wa kiroho kati yetu. Mitindo na desturi za kidunia, kiburi, kupenda starehe, kupenda kujionesha, kutokuwa na kiasi katika mavazi, nyumba na katika ardhi haya yananyang’anya kile ambacho kilipaswa kuwa katika hazina ya Mungu, na kukigeuzia katika kujiridhisha nafsi kile ambacho kingetumika katika kupeleka nuru ya kweli kwa ulimwengu. . .Mar 51.4

    Watoto wa nuru ambao ni wa mchana hawapaswi kujizingira na vivuli vya giza ambavyo vinakwenda na watendaji wa udhalimu. Badala yake, wanapaswa kusimama kwa uaminifu katika zamu zao wakiwa kama wabebaji wa nuru, wakikusanya nuru toka kwa Mungu ili kuisambaza kwa wale walio gizani. Mungu anataka watu wake wadumishe uadilifu, hila kugusa - yaani wasiige- mazoea ya wasiomcha Mungu.Mar 51.5

    Katika ulimwengu huu, Wakristo watakuwa “taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu,” wakionesha sifa zake Yeye aliyewaita “watoke gizani na waingie katika nuru yake ya ajabu.” Nuru hii haipaswi kuwa hafifu, hali itazidi kung’aa hadi katika siku ya ukamilifu. . . Ukweli unaofurahisha ambao umekuwa ukisikika masikioni mwetu kwa miaka mingi, “Bwana yuko karibu; iweni tayari,” ni ukweli wenye umuhimu zaidi leo kuliko wakati tulipousikia kwa mara ya kwanza.Mar 51.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents