Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kusimikwa kwa Sheria ya Jumapili, Sura ya 178

  Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa jina langu. Mathayo 24:9.Mar 186.1

  Wakali msukumo wa sheria ya Jumapili unapokuwa mkubwa zaidi na kukubalika, sheria itasimikwa dhidi ya washika amri. Watatishiwa kwa faini na magereza, na wengine wataahidiwa nafasi za madaraka, na zawadi nyingine na mafao kama vishawishi ili waikane imani yao. Lakini jibu lao la kudumu litakuwa: “Tuoneshe kosa letu kutoka katika neno la Mungu. .” Wale watakaokamatwa na kupelekwa mbele ya mahakama watatoa majibu ya nguvu kabisa kuuthibitisha ukweli, na baadhi ya wale watakaokuwa wakiwasikiliza watafanya uamuzi kushika amri zote za Mungu. Kwa namna hiyo nuru italetwa mbele ya maelfu ambao wasingepata kujua kweli hizi kwa namna nyingine yoyote ile.Mar 186.2

  Utiifu kwa neno la Mungu unaoambatana na uangalifu wa pekee utaonekana kuwa ni uasi. Mzazi aliyepofushwa na Shetani, atakuwa mkali sana kwa mtoto anayeamini; mabwana na mabibi watawaonea watumishi wanaozishika amri. Upendo utaondolewa; watoto watakanwa na kufukuzwa toka nyumbani. Maneno ya Paulo yatatimia dhahiri kama alivyosema: “wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.” 2 Tim. 3:12. Wale wanaoitetea kweli wanapokataa kuheshimu sabato ya Jumapili, baadhi yao watatupwa gerezani, wengine watawekwa uhamishoni, na baadhi watatendewa kama watumwa. . . .Mar 186.3

  Katika wakati huu wa mateso imani za watumishi wa Bwana zitajaribiwa. Watakuwa wametoa onyo kwa uaminifu, wakimtazamia Mungu na neno lake pekee. Roho wa Mungu, akiendelea kufanya kazi mioyoni mwao, atakuwa amewasukuma kunena. . . Hata hivyo, wakati dhoruba ya upinzani na shutuma zikiwakabiIi, baadhi wakiwa wamezidiwa na hofu kuu watatamka: “Kama tungeona mbele kwa matokeo ya maneno yetu, tungekaa kimya.” Watakuwa wamezingirwa na matatizo. Shetani atawakabili na majaribu ya kutisha. Kazi ambayo wameikubali itaonekana kuwa ngumu mno kuliko uwezo wao. Watatishiwa kuangamizwa. Msisimko uliowainua sasa utakuwa umekwisha; na bado hawataweza kurudi nyuma. Kisha, hali wakihisi hitaji lao kubwa sana, watakimbia kwa Mwenyezi ili wapate nguvu.Mar 186.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents