Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shetani Anazidisha Juhudi, Sura ya 122

  Malaika wa Bwana hufanya kituo, akiwazungukia wamchao na kuwaokoa. Zaburi 34:7.Mar 130.1

  Nguvu na chuki ya Shetani pamoja na majeshi yake ingetutisha kweli kama tusingekuwa tunaweza kupata kimbilio na wokovu katika nguvu ya Mkombozi wetu ambayo ni kubwa zaidi. Mara nyingi huwa tunazifunga nyumba zetu kwa makomeo na makufuli kulinda mali na maisha yetu dhidi ya watu wabaya; lakini mara nyingi hatufikirii juu ya malaika waovu ambao kila wakati wanatafuta kutufikia, na ambao hatuna njia ya kujilinda kwa nguvu zetu wenyewe dhidi yao. Wakiruhusiwa wanaweza kuyumbisha akili zetu, kuharibu na kutesa miili yetu, kuharibu mali na maisha yetu. Furaha yao pekee ni katika mateso na uharibifu. Hali ya wale wanaopinga matakwa ya Mungu na kusalimu amri kwa majaribu ya Shetani, mpaka Mungu awaache chini ya utawala wa pepo wabaya. Lakini wale wanaomfuata Kristo wako salama siku zote wakiwa chini ya ulinzi wake. Malaika wenye nguvu zaidi huwa wanatumwa kutoka mbinguni kuja kuwalinda. Yule mwovu hawezi kupenya katika ulinzi ambao Mungu amewawekea watu wake.Mar 130.2

  Vita kuu kati ya Kristo na Shetani, ambayo imeendelea kwa takriban miaka elfu sita sasa, itakwisha hivi karibuni; na yule Mwovu anazidisha juhudi zake kuiharibu kazi ya Kristo iliyofanyika kwa niaba ya mwanadamu na kuwafunga watu katika mitego yake. Kusudi analotaka kulitimiza ni kuwaweka watu katika giza na kutokuwa na toba mpaka maombezi ya Mwokozi yatakapofikia mwisho.Mar 130.3

  Juhudi maalum zisipofanyika kuzipinga nguvu za mwovu, kutokujali kunapotawala kanisani na katika ulimwengu, Shetani hasumbuki; kwani hayuko hatarini kupoteza wale aliowateka. Lakini akili zikielekezwa katika mambo ya milele, na roho zikawa zikiuliza, “Nifanye nini ili nipate kuokoka?” Mwovu anakuwa tayari, akitaka kupambanisha nguvu yake na ile ya Kristo.... Watu wanapokusanyika kumwabudu Mungu huwa anajihudhurisha. Ingawa haonekani, huwa anafanya kazi kwa umakini mkubwa kutawala akili za wale wanaoabudu.Mar 130.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents