Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kampeni ya Mwisho ya Shetani, Sura ya 56

    Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. 1 Yohana 2:18Mar 64.1

    Adui anajiandaa kwa ajili ya kampeni yake ya mwisho dhidi ya kanisa. Amejificha sana asionekane na watu kiasi kwamba wengi hawafikiri ya kwamba anaishi, na vivyo hivyo, wengi hawatambui shughuli na ukubwa wa uwezo wake. . .Mar 64.2

    Mwanadamu ni mateka wa Shetani na kwa asili anafuata mapendekezo na matashi yake. Ndani yake hakuna nguvu ya kupinga na kuukataa uovu. Ni pale tu Kristo anapokuwa ndani yake kwa imani iliyo hai...ambapo mwanadamu anaweza kudiriki kumkabili huyu adui mbaya sana. Namna yoyote nyingine ya kujilinda haifai kabisa. Ni kupitia kwa Kristo peke yake ndipo uwezo wa Shetani unazuiwa. Huu ni ukweli wa muhimu sana ambao wote wanapaswa kuuelewa. Shetani anashughulika sana kila wakati, akienda huku na kule, akipanda na kushuka duniani, akitafuta mtu ammeze. Lakini ombi la dhati la imani litachanganya jitihada zake hata zile zenye nguvu sana...Mar 64.3

    Shetani anategemea kuwahusisha masalio wa Mungu kwa ujumla katika maangamizi yanayokuja katika dunia. Wakati kuja kwa Kristo kunapokaribia, yeye (Shetani) atazidisha azma yake na uthabiti katika jitihada ya kuwaangusha. Wanaume kwa wanawake watainuka wakidai kuwa na nuru mpya au ufunuo mpya ambao kwa kawaida unavuruga imani ambayo imekuwako katika misingi imara siku zote. Hata ingawa mafundisho yao hayatakuwa na vithibitisho vya neno la Mungu, bado roho zitadanganywa. Taarifa za uongo zitasambazwa, na baadhi watanaswa katika mtego huu... Hatuwezi kuwa wazembe katika kuangalia aina yoyote ile ya makosa, kwani Shetani anadumu kutafuta namna ya kuwavuta watu toka katika ukweli...Mar 64.4

    Wapo watu ambao hawako imara kitabia. Wako kama donge la tope la udongo wa mfinyanzi ambalo laweza kuumbwa katika mwonekano wowote. . . Udhaifu huu, kukosa maamuzi, kutokuwajibika, vyapaswa vishindwe. Katika tabia ya kweli ya Ukristo ipo hali ya ujasiri usio wa kawaida ambao hauwezi kutengenezwa au kushushwa hata hali iwe mbaya kiasi gani. Watu wanapaswa kuwa na msimamo katika maadili, unyofu ambao hauwezi kubezwa, kuhongwa au kutishwa. . .Mar 64.5

    Mungu ameweka mipaka ambayo Shetani hawezi kuipita. Imani yetu iliyo takatifu sana ndiyo mipaka; na kama tutajijenga wenyewe zaidi katika imani, basi tutakuwa salama katika utunzaji unaotoka kwa Mwenyezi.Mar 64.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents