Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Vazi Jeupe Linahitajika, Sura ya 70

  Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi. Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Mathayo 22:11,12.Mar 78.1

  Tabia isiyo na mawaa watakayokuwa nayo wafuasi wa kweli wa Kristo inawakilishwa na vazi la arusi katika mfano. Kanisa limepewa “kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi,” “lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo.” Ufu. 19:8; Efe.5:27. Kitani nzuri, Maandiko yanasema, “ni matendo ya haki ya watakatifu.” Ufu. 19:8. Hii ni haki ya Kristo, tabia yake isiyo na kasoro, ambayo kwa njia ya imani anawapa wote wampokeao Yeye kama Mwokozi wao binafsi.Mar 78.2

  Vazi jeupe lisilo na hatia lilivaliwa na wazazi wetu wa kwanza wakati walipowekwa na Mungu katika Edeni takatifu. . . Lakini wakati dhambi iIipoingia, muunganiko na Mungu ulikatika, na nuru iliyokuwa imewazingira ikaondoka.... Mtu hawezi kufanya chochote ili kujaza nafasi ya vazi lake lisilo na hatia ambalo limepotea... Ni vazi pekee la Kristo mwenyewe ambalo amelitoa, liwezalo kutufanya tufikie kiwango cha kustahili kuwa mbele za Mungu. Kristo atavisha kila roho inayotubu, na kuamini.... Vazi hili, ambalo limefumwa katika mwonekano wa mbinguni, halina hata uzi mmoja utokanao na ubunifu wa kibinadamu. Katika ubinadamu wake, Kristo aliiweka tabia iliyo kamili, na Yeye anatupatia tabia hii. “Matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi.” Isa. 64:6. Kila kitu ambacho sisi wenyewe tunaweza kufanya kimenajisiwa kwa dhambi. Lakini Mwana wa Mungu “yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.” 1 Yoh. 3:5. . .Mar 78.3

  Kwa utii wake ulio mkamilifu amefanya iwezekane kwa kila mtu kutii amri za Mungu. Tunapojikabidhi kwa Kristo, moyo unaunganishwa na moyo wake, nia zetu zinaunganishwa na nia yake, mawazo yana kuwa mamoja na yake, fikira hutekwa naye; tunaishi maisha yake. Hiki ndicho kinachomaanishwa kwa kuvikwa vazi la haki yake. Ndipo Bwana anapotutazama, haoni vazi la majani ya mtini, haoni uchi wetu na ulemavu wa dhambi, lakini vazi lake mwenyewe la haki, ambalo ni utii kamili kwa sheria ya Yehova.Mar 78.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents