Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shetani na Umoja wa Watatu, Sura ya 183

  Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake. Ufunuo 13:4.Mar 191.1

  Alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.” Ingawa watajiita kuwa wafuasi wa Mwana-Kondoo wa Mungu, watu hawa wataingiwa na roho ya joka. Hawa watadai kuwa wanyenyekevu na wapole lakini watanena na kutekeleza sheria kwa roho wa Shetani, hivyo wakionesha kwa matendo yao ya kwamba wapo kinyume na kile wanachodai kujiita. Mamlaka hii iliyo kama Mwana- Kondoo itaunganika na joka katika kufanya vita dhidi ya wale wazishikao amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo. Shetani ataungana na Waprotestanti na wale wenye kumwamini Papa, akitenda kazi kwa umoja nao kama mungu wa dunia hii, akiamuru watu kana kwamba ni raia wa ufalme wake, akiwatendea na kuwatawala na kuwaongoza kama apendavyo. Kama watu hawatakubali kuzikanyaga amri za Mungu, roho wa joka atadhihirishwa. Hawa watatiwa gerezani, wataletwa mbele ya mabaraza, na kupigwa faini. “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao.” “akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasiosujudu sanamu ya mnyama wauawe.” Kwa namna hiyo, Shetani atajitwalia haki iliyo ya Yehova. Mtu wa dhambi ataketi katika kiti cha Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ni mungu, tena akijifanya kuwa zaidi ya Mungu.Mar 191.2

  Kuna tofauti iliyo wazi kati ya wale wenye muhuri wa Mungu na wale wamwabuduo mnyama na sanamu yake. Watumishi waaminifu wa Bwana watapokea mateso makali sana kutoka kwa waalimu wa uongo, ambao hawatasikiliza neno la Mungu, na ambao wanaandaa vikwazo vya kuwawekea wale ambao wanalisikiliza. Lakini watu wa Mungu hawapaswi kuogopa. Shetani hawezi kutenda kuliko mipaka yake. Bwana atakuwa ulinzi kwa watu wake. Majeraha wanayopewa watumishi wake kwa sababu ya kweli, anayahesabu kama yake Mwenyewe. Uamuzi wa mwisho utakapokuwa limefanyika, wakati wote watakapokuwa wameamua upande watakao kuwa, ama kwa Kristo na amri au kwa uasi mkuu, Mungu atainuka katika uweza wake na vinywa vya wale ambao wamemkufuru vitafumbwa milele. Kila aina ya mamlaka ambayo itakuwa imempinga itapokea adhabu yake.Mar 191.3

  *****

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents