Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuwa Tayari Kujibu, Sura ya 37

    Mwe tayari sikuzote kumujibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. 1 Petro 3:15Mar 45.1

    Nimeoneshwa kwamba wengi wanaodai kuwa na ufahamu wa ukweli wa leo hawajui kile wanachopaswa kukiamini. Hawajaelewa vithibitisho vya imani yao. Hawatambui kwa undani kazi ipaswayo kufanywa wakati huu. Wakati wa jaribio utakapofika, wapo watu ambao sasa wanahubiri wengine, ambao watajua, tathmini ya misimamo yao itakapofanyika, ya kwamba kuna mambo mengi ambayo hawawezi kuyafafanua vya kutosha. Kabla ya kujaribiwa huko, hawawezi kufahamu kutokujua kwao. Wapo wengi kanisani ambao bila kujali kujichunguza kwa makini wanafikiri wanaelewa kile wanachodai kukiamini; lakini, watajua udhaifu wao hapo pambano litakapozidi. Watakapotenganishwa na wenzao katika imani na kulazimika kusimama peke yao ili kueleza wanachokiamini, watashangaa kujiona jinsi walivyochanganyikiwa katika mawazo ya ukweli walioukubali. . .Mar 45.2

    Munguatainua watu wake; kama njia zingine zikishindikana, mafundisho potofu yatawaingilia, ambayo yatawachekecha, na kutenganisha makapi na ngano. Bwana anaita wote ambao wanaamini katika neno lake waamke toka usingizini. Nuru ya thamani imekuja, inayostahili kwa wakati huu.Mar 45.3

    . . Waumini hawapaswi kujifariji kwa dhana za makisio na zisizoelezeka vema zisadikiwazo kuwa kweli. Imani yao inapaswa ijikite ikiwa imara katika msingi wa neno la Mungu ili kwamba wakati wa jaribio ukifrka nao wakisimamishwa mbele za mabaraza kujibu maswali juu ya imani yao, waweze kutoa sababu za tumaini walilo nalo, kwa upole na kwa hofu.Mar 45.4

    Watumishi wa Kristo hawapaswi kuandaa hotuba ya kutoa wakati watakaposimamishwa katika jaribio la imani yao. Matayarisho yao yapaswa kufanywa siku kwa siku, wanapoweka hazina za neno la kweli la thamani la Mungu ndani ya mioyo yao, wakijilisha mafundisho ya Kristo, na kwa njia ya sala wakiimarisha imani yao; ndipo, hapo watakapoletwa katika jaribio, Roho Mtakatifu atawaletea katika kumbukumbu zao kweli zile zitakazogusa mioyo ya wale watakokuja kusikiliza.Mar 45.5

    Kufumba na kufumbua, Mungu atawaletea mawazoni mwao ujuzi walioupata katika kuchunguza Maandiko, katika wakati huo huo unapohitajika.Mar 45.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents