Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kinga Dhidi ya Kila Jaribu, Sura ya 83

    Basi Jitoeni wenyewe kwa Mungu,.. . na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi. Warumi 6:13,14.Mar 91.1

    Ipo nguvu moja tu iwezayo kuvunja mvuto wa uovu katika mioyo ya watu, na hiyo si nyingine bali ya Mungu katika Kristo Yesu . . . Neema yake pekee yaweza kutupa sisi nguvu ya kupinga na kutawala mielekeo ya asili yetu iliyoharibika.Mar 91.2

    Thamani ya milele ya kafara iliyohitajika kwa ajili ya ukombozi wetu inafunua ukweli ya kwamba dhambi ni uovu wa kutisha. Kwa sababu ya dhambi mwanadamu kama kiumbe ameharibiwa, mawazo yake yamepotoshwa, na tafakuri zake zimechafuliwa. Dhambi imeshusha uwezo wa roho. Majaribu yajapo tokea nje huitikiwa na hisia itokayo moyoni, kisha miguu hugeuka bila kuelewa kuelekea katika uovu. Kama jinsi ambavyo kafara kwa niaba yetu ilivyokuwa kamili, vivyo hivyo urejeshwaji wetu toka katika kuchafuliwa na dhambi unapaswa kuwa kamili. Hakuna tendo la uovu ambalo sheria italifumbia macho; hakuna tendo lolote lisilo haki ambalo litakwepa hukumu ya sheria. Maisha ya Kristo yalikuwa utimilifu kamili wa kila kanuni ya sheria. Alisema, “nime.. shika amri za Baba yangu...” Yn. 15:10. Maisha yake ni kiwango cha utii na huduma.Mar 91.3

    Leo Shetani anawasilisha majaribu yaleyale aliyoyawasilisha kwa Kristo, akitupatia falme za dunia badala ya utii wetu kwa Mungu. Lakini kwake yeye amtazamaye Yesu kama mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yake, majaribu ya Shetani hay ana nguvu. Hawezi kumfanya atende dhambi yeye ambaye amekubali kwa imani tabia ya yule ambaye alijaribiwa kwa namna zote kama sisi, na wala hakutenda dhambi.Mar 91.4

    Tendo la kufukuza dhambi huwa linafanyika ndani ya roho yenyewe. Ni kweli kwamba sisi hatuna nguvu ya kutuweka huru dhidi ya nguvu za Shetani: lakini tunapotamani kuwekwa huru na dhambi, na katika uhitaji wetu tunapoliIia uwezo ulio juu kuliko sisi, nguvu za roho zetu hujazwa na uwezo wa kimbingu wa Roho Mtakatifu, na hivyo roho hutii matashi ya Roho Mtakatifu katika kutimiza mapenzi ya Mungu.Mar 91.5

    Mungu anahitaji watu waliojasiri katika kutenda mema, watakaosimama kwa ujasiri katika uchafu wa kizazi hiki kilichopotoka. Kutakuwa na watu ambao watashikilia nguvu za kimbingu bila kukoma kiasi cha kuwa uthibitisho dhidi ya kila jaribu.Mar 91.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents