Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ukweli Utashinda, Sura ya 10

    Na yule malaika ... akaapa kwa Yeye aliye hai hata milele na milele ... ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya. Ufunuo 10:5, 6.Mar 18.1

    Ujumbe wa Ufunuo 14, unaotangaza kuwa saa ya hukumu ya Mungu imekuja, unatolewa katika wakati wa mwisho; na malaika wa Ufunuo 10 anaonekana akiwa amekanyaga baharini kwa mguu mmoja, na nchi kavu kwa mguu mwingine, ikimaanisha kuwa ujumbe huu utakwenda hata nchi za mbali, bahari itavukwa, na visiwa vya baharini vitasikia ujumbe wa onyo la mwisho ukitangazwa....Mar 18.2

    “Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni, akaapa kwa Yeye aliye hai milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya” (Ufu. 10:5, 6). Ujumbe huu unatangaza mwisho wa vipindi vya unabii. Kutokutimia kwa matarajio ya wale ambao walikuwa wanatarajia kumwona Bwana wetu mwaka 1844, kulileta uchungu sana kwa wale waliokuwa wamesubiri kwa shauku kubwa kuonekana kwake. Mungu alikuwa amekusudia kwamba matarajio hayo yasitimie....Mar 18.3

    Hakuna wingu lililowahi kulifunika kanisa ambalo Mungu hakulifanyia maandalizi; hakuna hata jambo moja lililo kinyume na kazi ya Mungu ambalo Mungu hakuliona tangu mwanzo. Mambo yote yametokea sawasawa na vile alivyotabiri kwa njia ya manabii wake. Hajaliacha kanisa lake gizani, lakini ameyaeleza kwa ufasaha katika unabii yale ambayo yatatokea, na kwa mkono wake, ukifanya kazi kwa wakati ulioamriwa, ameyatimiza yale ambayo Roho wake Mtakatifu alikuwa amewavuvia manabii kuyatabiri. Makusudi yake yote yatatimia na kusimama. Sheria yake inahusiana na kiti chake cha enzi, na mawakala wa Shetani, pamoja na wale wa wanadamu hawawezi kuishinda. Ukweli huvuviwa na kulindwa na Mungu; utadumu, na utafaulu, ingawa wakati mwingine unaweza kuonekana kana kwamba umefunikwa na giza. Injili ya Kristo ni sheria ambayo inaonekana katika tabia. Uongo unaotendeka kinyume cha sheria hiyo, kila njama za kuuthibitisha uongo, kila udanganyifu uliotengenezwa na mawakala wa Shetani, hatimaye utashindwa milele, na ushindi wa ukweli utaonekana kama jua linavyoonekana adhuhuri. Jua la haki litaangaza, lenye kuponya katika mbawa zake na dunia yote itajaa utukufu wake.Mar 18.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents