Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Umizimu na Sheria ya Jumapili, Sura ya 159

  “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isaya 8:20.Mar 167.1

  Nguvu ya miujiza inayodhihirishwa kupitia umizimu itaweka mvuto wake dhidi ya wale wanaochagua kumtii Mungu kuliko wanadamu. Mawasiliano toka kwa pepo wachafu yatatangaza kuwa Mungu amewatuma kuwashawishi wapingaji wa ibada ya Jumapili kwamba wamekosea, na kuwathibitishia kuwa sheria za nchi sharti zitiiwe sawa na sheria za Mungu. Wataombolezea uovu mkuu unaoendelea duniani na kuunga mkono ushuhuda wa walimu wa kidini kwamba mmomonyoko wa maadili umesababishwa na kuinajisi Jumapili. Chuki kuu itaibuliwa dhidi ya wote wanaoukataa ushuhuda wao.Mar 167.2

  Wale wenye kupinga mafundisho ya umizimu wanachokoza, siyo tu wanadamu, ila Shetani na malaika zake. Wamejiunga katika pambano dhidi ya “falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” (Efe. 6:12). Shetani hatasalimu amri hadi pale atakaposu kumiwa mbali kwa nguvu kuu za wajumbe wa mbinguni. Watu wa Mungu wanapaswa kumkabili, kama alivyofanya Mwokozi, kwa maneno: “Imeandikwa.” Shetani anaweza kunukuu Maandiko sasa kama alivyofanya siku za Kristo, naye atayapotosha mafundisho ya Biblia ili yapate kukumbatia udanganyifu wake. Wale ambao watasimama wakati wa hatari kubwa sharti waelewe vyema ushuhuda wa Maandiko. {Maranatha 167.2}Mar 167.3

  Wengi watakabiliwa na roho za pepo wachafu zikiwakilisha sura za jamaa ama marafiki na kutangaza uzushi hatari kabisa. Wageni hawa watashawishi kutaka huruma zetu na kutenda miujiza kuwafanya watu wasadiki uongo wao. Twapaswa kujiandaa kuwapinga kwa ukweli wa Biblia kwamba wafu hawajui neno lo lote na kwamba wale watakaojitokeza kwa hakika ni roho za pepo wachafu. {Maranatha 167.3}Mar 167.4

  Mawakala wa Shetani walio katika umbo la mwanadamu watashiriki katika pambano hili kuu la mwisho kupinga ujenzi wa ufalme wa Mungu. Malaika wa Mungu wakiwa wakiwa katika sura za wanadamu watakuwa kwenye uwanja wa mapambano. Pande mbili zinazokinzana zitaendelea kuwepo hadi kufungwa kwa sura kuu ya mwisho ya historia ya ulimwengu huu. {Maranatha 167.4}Mar 167.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents