Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uamsho wa Bandia, Sura ya 25

    Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nayakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wanye kiburi wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukurani, wasio safi, ... wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake: hao nao ujiepushe nao. 2 Timotheo 3:1, 2, 5.Mar 33.1

    Kabla ya mapigo ya Mungu juu ya dunia, miongoni mwa watu wa Bwana, kutakuwa na uamsho wa aina ile ya mwanzo, ambao haujawahi kuonekana tangu enzi za mitume. Roho na uweza wa Mungu utamiminwa juu ya watoto wake. Wakati huo wengi watajitenga na makanisa ambamo kuipenda dunia kumechukua nafasi ya kumpenda Mungu. Wengi WAO, wachungaji na washiriki, watapokea kwa furaha ukweli ambao Mungu ameufanya utangazwe wakati huu ili kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio wa pili wa Bwana. Adui wa roho anataka kuikwamisha kazi hii; na kabla wakati wa harakati hizo haujafika, atajaribu kuizuia kwa kuanzisha uamsho wa bandia. Katika makanisa ambayo anaweza kuyaweka chini ya uwezo wake wa kudanganya, atafanya ionekane kana kwamba mibaraka maalum ya Mungu imemwagwa; itaonekana kana kwamba kuna vuguvugu kubwa la kidini. Wengi watajigamba kuwa Mungu anawafanyia makuu, wakati kazi hiyo itakuwa ni ya roho nyingine. Shetani atajaribu kueneza ushawishi wake juu ulimwengu wa Kikristo kwa kutumia dini.Mar 33.2

    Katika uamsho mwingi uliotokea katika nusu karne iliyopita, ushawishi huo huo umekuwa ukifanya kazi, ambao kwa namna moja au nyingine, utaonekana kwa kiwango cha juu zaidi katika harakati zijazo. Kutakuwa na msisimko wa hisia, uchanganyaji wa ukweli na uongo, ambao umetengenezwa ili kudanganya. Lakini hakuna haja ya kudanganyika. Katika nuru ya neno la Mungu si vigumu kutambua asili ya harakati hizo. Po pote watu wanapopuuza ushuhuda wa Biblia, na kuuacha ukweli wa wazi, unaohitaji kujikana nafsi na kuukana ulimwengu, tunaweza kuwa na uhakika kuwa baraka za Mungu hazijawekwa kwao. Na kwa kanuni ambayo Kristo mwenyewe aliitoa, “Mtawajua kwa matunda yao” (Mt. 7:16), itaonekana wazi kuwa harakati hizo si kazi ya Roho wa Mungu.Mar 33.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents