Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Umoja wa Kidini wa Watatu, Sura ya 182

  Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote, kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. Ufunuo 16:13,14.Mar 190.1

  Kwa tamko Iinaloshinikiza taasisi ya upapa katika kuvunja sheria ya Mungu, taifa letu [Marekani] litajitenga lenyewe kikamilifu kutoka katika haki. Wakati Uprotestanti utakaponyoosha mkono wake hadi ng’ambo ya ghuba ili kukamata mkono wa mamlaka ya Kirumi, wakati utakaponyoosha mikono kuvuka rima kuu ili kushikana na umizimu, na mvuto wa muunganiko wa mifumo mitatu, nchi yetu itakana kila kanuni ya Katiba yake kama serikali ya Kiprotestanti na Ki-jamhuri, na hivyo kutoa nafasi kwa ajili ya kutangazwa kwa uongo wa upapa na ghiliba zake, ndipo tutakapojua ya kwamba wakati umewadia kwa ajili ya matendo ya ajabu ya Shetani na kwamba mwisho umekaribia.Mar 190.2

  Kupitia katika makosa mawili makuu, dhana ya roho kutokufa na utakatifu wa Jumapili, shetani atawavuta na kuwadanganya watu. Wakati dhana hiyo ya roho kutokufa inaweka msingi wa umizimu, hilo la pili la utakatifu wa Jumapili, litafanya muunganiko wa kihisia na Rumi. Waprotestanti wa Marekani watakuwa mbele kabisa kunyoosha mikono yao hadi ng’ambo ya ghuba ili kukamata mkono wa umizimu; mikono yao itapita juu ya Ule rima kuu ili kushikana na mamlaka ya Kirumi; na kutokana na mvuto wa umoja wa watatu hawa, nchi hii itafuata nyayo za Rumi katika kukanyaga haki za dhamiri za watu. . .Mar 190.3

  Waungao mkono Upapa, Waprotestanti na watu wa tawala za kidunia watakubaliana na mfumo wa utauwa usio na nguvu na wataona umoja huu kama msukumo mkuu kwa ajili ya kuongoa ulimwengu na kukaribisha milenia ambayo imesubiriwa kwa muda mrefu sana.Mar 190.4

  Kwa kitendo cha taifa letu [Marekani] kukana kanuni za serikali yake kiasi cha kutekeleza sheria ya Jumapili, Uprotestanti utakuwa umeungana mikono na upapa; na hiki kitakuwa kitendo cha hakika cha kuhuisha uonevu ambao kwa muda mrefu umekuwa ukitafuta fursa ya kuinuka tena na kutawala kidhalimu.Mar 190.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents