Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maandiko: Kinga Yetu, Sura ya 87

    Je, hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? Waebrania 1:14.Mar 95.1

    Kadiri watu wa Mungu wanavyodumu katika uaminifu kwake, kadiri wanavyojishikamanisha kwa imani iliyo hai katika Yesu, wanakuwa chini ya ulinzi wa malaika wa mbinguni, na Shetani hataruhusiwa kuendeleza usanii wake mwovu juu yao hadi maangamizi. Lakini wale wanaoruhusu dhambi iwatenge na Kristo wamo katika hatari kuu. . .Mar 95.2

    Shetani sasa yuko katika jitihada ya dhati katika kucheza na uhai wa roho za watu kuliko wakati wowote uliopita; na kama tusipodumu kuwa macho, atajenga mioyoni mwetu, kiburi, kujipenda nafsi, kupenda dunia, na tabia nyingine nyingi mbovu. Atatumia pia kila nyenzo kwa ajili ya kulegeza imani yetu kwa Mungu na vilevile atalegeza imani yetu kwa kweli za Neno lake. Kama hatuna uzoefu wa ndani katika mambo ya Mungu, kama hatuna ujuzi wa kutosha wa Neno la Mungu, tutaghilibiwa na hoja za uongo zitokanazo na makosa na hila za adui. Mafundisho ya uongo yatadhoofisha misingi ya wengi, kwa sababu hawajazoea kutengenisha ukweli toka kwa uongo. Kinga yetu pekee dhidi ya hila za Shetani ni kujifunza Maandiko kwa bidii, kuwa na uelewa wa juu kuhusu sababu za imani yetu, na kwa uaminifu kutekeleza kila wajibu tunaoujua. Kuendekeza dhambi moja inayojulikana kwa mtu husika kutasababisha udhaifu na giza, na kutuweka chini ya majaribu makali. . .Mar 95.3

    Je, tunafungua mlango wa moyo kwa Yesu, na kufunga kila namna ya mapito yawezayo kutumiwa na Shetani? Je, tunapata kila siku nuru ing’aayo zaidi, nguvu zaidi ili tupate kusimama katika haki ya Kristo? Je, tunasafishwa mioyo yetu toka katika ubinafsi wote, na kutakaswa, ikiwa maandalizi ya kupokea mvua ya masika toka mbinguni?. . .Mar 95.4

    Kazi ya ushindi ni kazi iliyo kuu. Je, tutaishikilia kwa nguvu na kwa subira? Kama tusipotenda hivyo, hatutaondolewa “mavazi yetu machafu”. Kamwe hatupaswi kutegemea ya kwamba tutavuliwa haya mavazi kwa nguvu; sharti sisi wenyewe tuoneshe kwanza tamaa ya kuyavua. Tunapaswa kutafuta namna ya kujitenga na dhambi, tukitegemea ustahili wa damu ya Kristo; na kisha katika siku ya mateso, wakati adui akiweka shinikizo dhidi yetu, nitatembea kati ya malaika.Mar 95.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents