Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ushupavu wa Dini na Kunena kwa Lugha, Sura ya 146

  “Na roho za manabii huwatii manabii. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.” 1 Wakorintho 14:32,33.Mar 154.1

  Roho ya ushupavu wa dini imetawala kundi fulani la washika Sabato ... Wamekunywa kidogo tu katika chemchemi ya ukweli na hawana ujuzi wa roho ya ujumbe wa malaika wa tatu. Hakuna kitu cho chote kinachoweza kufanyika kwa ajili ya kundi hili hadi pale mtazamo wao wa ushupavu wa dini utakapokuwa umerekebishwa.Mar 154.2

  Baadhi ya watu hao wanafanyia mazoezi kile ambacho wanakiita karama na kusema kwamba Bwana ameviweka kanisani. Wanatamka maneno ambayo hayaeleweki na yasiyo na maana ambayo wanayaita kuwa ni lugha isiyojulikana, ambayo siyo kwamba haijulikani kwa wanadamu tu, bali hata kwa Bwana na mbingu yote. Karama kama hizo zinaanzishwa na wanadamu huku wakiwa wanasaidiwa na yule mdanganyifu mkuu. Ushupavu wa dini, msisimko bandia, kunena kwa lugha ambako ni kwa bandia, na mazoezi ya makelele, vimefikiriwa kuwa ni karama ambazo Mungu ameziweka ndani ya Kanisa. Baadhi wamedanganyika hapa. Matokeo ya mambo haya yote bado hayajawa mazuri ...Mar 154.3

  Wapo wengi ambao wamekosa utulivu na ambao hawatakubali nidhamu, mfumo na utaratibu. Wanafikiri kwamba uhuru wao utakuwa umepunguzwa iwapo wataweka kando maamuzi yao na kukubali maamuzi ya wale ambao wamekuwa na uzoefu kazini. Kazi ya Mungu haitaendelea mbele mpaka kuwepo na tabia ya kukubali utaratibu na kuondoa roho ya ushupavu wa dini katika mikutano yao, roho ambayo ni ya kutokujali na kutofuata utaratibu. Maoni na hisia siyo ushahidi wa hakika kuwa mtu huyo anaongozwa na Bwana. Kama asipotiIiwa mashaka, Shetani ataleta maoni na hisia. Maoni na hisia siyo viashiria salama. Wote wanapaswa kufahamu vizuri ushahidi wa imani yetu, na somo kuu linapaswa kuwa juu ya namna watakavyopamba imani yao na kuzaa matunda kwa utukufu wa Mungu. ... Roho ya uzembe, mzaha na upuuzi haina budi kukemewa. Siyo ushahidi wa neema ya Mungu katika mioyo ya watu ikiwa wahusika watanena na kuomba katika mikutano kwa kadiri ya talanta zao, na kisha wanapokuwa nje ya mkutano wakazungumza na kutenda ovyoovyo na kwa fujo. ...Mar 154.4

  Kamwe, kweli ya Mungu haitamshusha mtu hadhi, bali itamwinua juu mpokeaji, itamfanya kuwa na utambuzi safi, itatakasa maamuzi yake, na kumkamilisha kwa ajili ya ushirika wa malaika watakatifu katika ufalme wa Mungu.Mar 154.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents