Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kujitegemea Kimaadili, Sura ya 39

  Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi. 2 Wakorintho 6:17, 18Mar 47.1

  Wengi leo wana utando katika nyuso zao. Utando huu ni mapenzi ya desturi na kawaida za kidunia, ambazo huwaficha mbali na utukufu wa Bwana. Ni tamaa ya Mungu ya kwamba tukaze macho yetu kwake, ili tusione mambo ya dunia hii.Mar 47.2

  Ukweli unapodhihirishwa kwa vitendo maishani, kiwango cha maisha kitainuka juu zaidi hata kulingana na matakwa ya Biblia. Hali hii italazimu kuwepo na upinzani dhidi ya mitindo, desturi, mazoea, na kanuni za kidunia. Mivuto ya kidunia, iliyo kama mawimbi ya bahari, inapiga dhidi ya wafuasi wa Kristo ili kuwasomba toka kwa kanuni za kweli za upole na neema yake; lakini yatupasa kusimama imara katika kanuni kama mwamba. Hili Iinahitaji ujasiri wa kimaadili kulifanya, na wale ambao roho zao hazijafungamana na Mwamba wa milele watasombwa na mkondo huu wa kidunia. Maisha yetu yakiwa yamefichwa ndani ya Mungu na Kristo, ndipo tu tunapoweza kusimama imara. Katika kupingana na dunia, kujitegemea kimaadili ndiyo njia pekee. Kwa knjikabidhi kikamilifu kwa mapenzi ya Mungu, tutawekwa mahali palipoinuka, na tutaona umuhimu wa maamuzi ya kujitenga na desturi na mazoea ya kidunia. Hatuitwi kuinua kiwango chetu juu kidogo tu kuzidi kile cha dunia, lakini tunaaitwa kufanya tofauti kati ya viwango hivi iwe dhahiri. . .Mar 47.3

  Si suala rahisi kupata hazina yenye thamani isiyoelezeka ya uzima wa milele. Hakuna awezaye kuipata huku akiendelea kuburuzwa na mkondo wa dunia. Anapaswa kusimama kinyume cha dunia na kujitenga na pia kutogusa uchafu. Hakuna awezaye kutenda kidunia bila kusombwa na mkondo wa dunia. Hakuna awezaye kufanya maendeleo ya kuelekea juu bila kuwa na juhudi iliyoambatana na uvumilivu. Yeye atakaye kushinda, anapaswa kumng’ang’ania Kristo. Asiangalie nyuma, lakini adumu kutazama juu, huku akiongeza neema juu ya neema. Hadhari ya mtu binafsi ndiyo gharama ya usalama wake. . .Mar 47.4

  Mwisho wa mambo yote umekaribia. Lipohitaji sasa la watu waliojiweka tayari na silaha za pambano kwa ajili ya Mungu.Mar 47.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents