Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mapambano ya Silaha Siku za Mwisho, Sura ya 166

    BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia. Yeremia 25:32.Mar 174.1

    Hivi karibuni sana taabu ya kutisha itainuka kati ya mataifa - taabu ambayo haitakoma hadi hapo Yesu atakapokuja. Yatupasa tuungane kwa umoja kuliko wakati wo wote uliopita, tukimtumikia Yeye ambaye ameandaa kiti chake cha enzi mbinguni na ambaye ufalme wake uko juu ya falme zote. Mungu hajawaacha watu wake na uwezo wetu linapatikana katika kutomwacha Yeye.Mar 174.2

    Hukumu za Mungu zipo duniani. Vita na tetesi za vita, uangamivu kwa njia ya moto na mafuriko, vyote vinaeleza wazi kuwa wakali wa taabu, ambao utaongezeka hadi mwisho, umekaribia sana na upo ukingoni. Hatuna muda wa kupoteza. Ulimwengu unatikiswa na roho ya vita. Unabii wa sura ya kumi na moja wa Danieli umekaribia kufikia utimilifu wake wa mwisho.Mar 174.3

    Siyo muda mrefu dhoruba kati ya mataifa itatokea kwa nguvu ambayo hatuitegemei kwa sasa. Wakati uliopo ni wakati wa kuwa makini sana kwa wote walio hai. Watawala na wakuu wa nchi, watu wanaoshikilia nafasi za heshima na mamlaka, watu wenye hekima wa viwango vyote, wameweka mtazamo wao katika matukio yanayotuzunguka. Wanatazama mataifa ambayo mahusiano yao siyo mazuri, na yamo katika hatari ya kuharibika . Wanatambua kuongezeka kwa kila namna ya kidunia, na wanaelewa kuwa jambo lililo muhimu sana tena kubwa linakaribia kutokea, kuwa ulimwengu upo katika ukingo wa zahama isiyo ya kawaida.Mar 174.4

    Tumekirimiwa na Mungu muda wa pumziko. Kila uwezo tunaopewa toka Mbinguni unapaswa utumike sasa katika kufanya kazi kwa ajili ya wale wanaopotea katika ujinga. Sharti tusichelewe. Kweli inapaswa kuhubiriwa katika sehemu zenye giza katika dunia. . . Kazi kubwa sharti ifanyike, na kazi hii imekabidhiwa wale waujuao ukweli kwa ajili ya wakati huu.Mar 174.5

    Katika hatua za mwisho za historia ya dunia hii, vita itainuka. Kutakuwa na maafa, na njaa. Maji yataumuka toka katika vina vyake na kugharikisha mipaka yake. Mali na maisha vitaharibiwa kwa moto na mafuriko. Tunapaswa kujiandaa kwa ajili ya makao makubwa ambayo Kristo amekwenda kuwaandalia wale wampendao. Hapo ndipo pa kupumzikia toka katika mapambano ya dunia.Mar 174.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents