Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Siri ya Maendeleo, Sura ya 78

    Enyi watu, mtumainini siku zote, ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu. Zaburi 62:8Mar 86.1

    Kama tunahitaji kufanya maendeleo katika maisha ya kimbingu sharti tuwe katika maombi mengi. Wakati ujumbe wa kweli lilipohubiriwa kwa mara ya kwanza, tulisali sana. Mara kwa mara sauti ya ombi la upatanisho lilisikika kutokea katika chumba, katika banda, katika bustani ya matunda, au katika kijisitu. Kila mara tulitumia wakati katika maombi ya dhati, kwa pamoja wawili au watatu tulidai ahadi; mara kwa mara sauti za kulia zilisikika na kisha sauti za shukrani na nyimbo za sifa. Sasa siku ya Mungu imekaribia sana kuliko pale tulipoanza kuamini, na hivyo tunapaswa kuwa makini zaidi, kukereketwa zaidi, na wenye juhudi zaidi ya zile siku za awali. Hatari kwetu leo ni kubwa kuliko wakati ule.Mar 86.2

    Ilikuwa katika saa za maombi ya faragha ambapo Yesu akiishi hapa duniani alipokea hekima na uweza. Hebu vijana wafuate kielelezo chake katika kupata nafasi tulivu alfajiri na jioni kwa ajili ya kuwasiliana na Baba yao aliye mbinguni. Vilevile, siku nzima na wainue mioyo yao kwa Mungu. Katika kila hatua ya njia yetu anasema, “mimi BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume,. . . Usiogope; mimi nitakusaidia. Isa. 41: 13. Kama watoto wetu wangeweza kujifunza somo hili mapema katika miaka yao ya awali, wangekuwa na upya wa maisha na uwezo, wangekuwa na furaha na burudani katika kuishi kwao!Mar 86.3

    Hebu moyo wako na uvunjike kwa kumhitaji Mungu, kwa ajili ya Mungu aliye hai. Maisha ya Kristo yameonesha kile ambacho ubinadamu waweza kutenda ukiwa limefanywa mwenza wa asili ya kimbingu. Yote ambayo Kristo aliyapokea toka kwa Mungu tunaweza kuwa nayo pia. Hivyo omba ili upokee. Ukiwa na imani ya Yakobo yenye subira, ukiwa na msimamo usioyumba wa Eliya, dai kwa ajili yako yote ambayo Mungu ameahidi.Mar 86.4

    Ruhusu maono yenye utukufu ya Mungu yajaze mawazo yako. Hebu maisha yako yafumwe kwa viunganishi vinavyokuunganisha na maisha ya Yesu. Yeye aliyeamuru kwamba nuru ing’ae gizani yuko tayari kung’aa moyoni mwako, kukupa nuru ya ujuzi wa utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. Roho Mtakatifu atachukua mambo ya Mungu na kukuonesha wewe.... Kristo atakuongoza hadi katika kingo za Umilele. Unaweza kuuona utukufu nyuma ya pazia, na kufunulia watu ukamilifu wake ambaye daima anaishi ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu.Mar 86.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents