Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Himiza Kuishi Kiafya, Sura ya 111

    Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Warumi 12:1.Mar 119.1

    Haiwezekani kwa mtu kuutoa mwili wake kama ibada iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, hali akiendelea kuendekeza mazoea yanayomzuia kuwa na nguvu kimwili, kiakili, na kimaadili. Kwa mara nyingine mtume anasema, “wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Rum. 12:2.Mar 119.2

    Tumo katika ulimwengu ambao haupatani na haki au usafi wa tabia, na hasa hasa kukua katika neema. Tunapotazama pote, tunaona machukizo na ufisadi, upotovu na dhambi. Haya yote ni maadui wakubwa wa kazi ipaswayo kukamilishwa ndani yetu mara kabla ya kupokea zawadi ya hali ya kutokufa! Wateule wa Mungu sharti wasimame bila kutikiswa kati ya ufisadi unaoongezeka ukiwazunguka katika siku hizi za mwisho. Sharti miili yao ifanywe kuwa mitakatifu, na roho zao zifanywe kuwa safi. Ili kazi hii ikamilishwe, yapasa ichukuliwe mara moja, kwa umakini na kwa kueleweka vema. Roho wa Mungu anapaswa kuwa mtawala kikamilifu, akiongoza kila tendo.Mar 119.3

    Matengenezo ya kiafya ni tawi moja la kazi kuu inayoambatana na watu kwa ajili ya kuja kwa Bwana... Watu hawawezi kuendelea kuvunja sheria za asili kwa kuendekeza tamaa mbaya katika lishe na mengine, bila kuvunja sheria ya Mungu. Kwa sababu hiyo, Mungu ameruhusu nuru ya matengenezo ya afya ing’ae kwetu, ili tupate kutambua ubaya wa kuvunja sheria ambazo Yeye ameziweka ndani yetu.Mar 119.4

    Kuweka wazi sheria za asili, na kusisitiza juu ya utii kwazo, ni kazi inayopelekana na ujumbe wa malaika yule wa tatu. . . Yeye (Mungu) amepanga kwamba somo hili lihamasishwe, na mawazo katika jamii yaamshwe kikamilifu kulichunguza; kwani haiwezekani kwa watu kuuthamini ukweli mtakatifu hali wakiwa wametawaliwa na nguvu ya mazoea ya dhambi yanayoua neva za bongo na afya kwa ujumla.Mar 119.5

    Yeye aipendaye nuru ya matengenezo ya kiafya ambayo Mungu amempatia, anao msaada mkubwa katika kazi ya kutakaswa katika kweli, na pia kuwekwa tayari kwa ajili ya hali ya kutokufa.Mar 119.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents