Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Shamba ni Ulimwengu, Sura ya 16

    Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mikiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Mathayo 28:19Mar 24.1

    Nilipokuwa California mwaka 1874, nilioteshwa ndoto ya kuvutia saa.... Niliota kwamba ndugu kadhaa wa California walikuwa katika halmashauri wakijadili mipango bora kwa ajili ya kazi katika msimu ujao....Mar 24.2

    Kijana mmoja ambaye nilikuwa nimemwona mara kwa mara katika ndoto zangu, alikuwa amekuja kwenye halmashauri. Alisikiliza kwa makini sana maneno yaliyokuwa yakisemwa, na kisha, akiongea kwa umakini na ujasiri wenye mamlaka, alisema:Mar 24.3

    “Miji na vijijji ni sehemu ya shamba la Bwana. Wanapaswa kuusikia ujumbe wa onyo. Adui wa ukweli anafanya kila juhudi kuwageuza watu kutoka kwenye ukweli wa Mungu kwenda kwenye uongo.... Mnapaswa kupanda kila palipo na maji.Mar 24.4

    Inawezekana msiyaone matunda ya kazi yenu, lakini jambo hilo lisiwakatishe tamaa. Mfuateni Kristo kama kielelezo. Alikuwa na wasikilizaji wengi, lakini wafuasi walikuwa wachache.”Mar 24.5

    Yule mjumbe aliendelea kusema: “Mnaendekeza mawazo finyu sana juu ya kazi ya wakati huu. Mnajaribu kuipangilia kazi kwa namna ambayo mnaweza kuibeba katika mikono yenu. Mnapaswa kuwa na mtazamo mpana zaidi. Nuru yenu haipaswi kuwekwa chini ya pishi au chini ya kitanda, bali kwenye kiango, ili iwaangazie wote walio katika nyumba. Nyumba yenu ni ulimwengu....Mar 24.6

    “Nchi nyingi zinasubiri nuru ya hali ya juu itokayo kwa Bwana: na imani yenu imepungua, ni ndogo sana. Mtazamo wenu juu ya kazi ya Mungu unapaswa kukuzwa.... Songeni mbele. Mungu atatenda kwa uwezo mkuu kama mkienenda katika unyenyekevu wa moyo mbele zake. Kuzungumzia yasiyowezekana ni kukosa imani. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Nuru ya matakwa ya lazima ya sheria ya Mungu itaupina... ulimwengu.”...Mar 24.7

    Muda ni mfupi; na wote wanaouamini ujumbe huu, wanapaswa kuuona wajibu muhimu walio nao wa kuwa watendakazi wasiotaka kujinufaisha, wakielekeza ushawishi wao mahali ulipokusudiwa, na kamwe wasionekane wakipingana na wale wanaotafuta kuiendeleza kazi ya Mungu....Nuru ambayo Mungu ametupatia haina thamani kubwa kwa ulimwengu kama isipoonekana kwa kutolewa mbele ya watu.Mar 24.8

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents