Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jihadharini na Watu Wanaowagawa, Sura ya 149

    “Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!” Luka 17:1.Mar 157.1

    Mungu anawaleta watu na kuwaandaa kusimama kama mtu mmoja, wakiwa na umoja, ili kunena mamoja, na kutekeleza ombi la Kristo kwa ajili ya wanafunzi wake. . . “Wote wawe na umoja: kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu . . ”Mar 157.2

    Kuna vikundi vidogo vidogo ambavyo daima vinatokea vinaamini kwamba Mungu yuko pamoja na watu wachache tu, ambao wametawanyika, na mvuto wao ni kuharibu na kutawanya kile ambacho watumishi wa Mungu wanajaribu kukijenga . . . Watu ambao wanafanya kila juhudi kulingana na neno la Mungu ili wapate kuwa kitu kimoja, na ambao wamethibitika katika ujumbe wa malaika wa tatu, wao wanawaangalia kwa mashaka kwa sababu tu kwamba wanaeneza utendaji wao wa kazi na kukusanya roho ili kujiunga na ukweli. Wanawaona kama watu wa ulimwengu, kwa sababu wana mvuto ulimwenguni . . .Mar 157.3

    Mtu mmoja anatokea akiwa anadai kwamba anaongozwa na Mungu, na mtu huyo anatetea wazo kuwa waovu hawatafufuka. . . Mwingine anashikilia maoni potofu kuhusu siku za usoni. ... Wote wanataka uhuru kamili wa kidini, na kila mmoja anafuata njia yake mwenyewe, na bado wanadai kuwa Mungu anatenda kazi miongoni mwao. Watu hawa hawana akili timamu; wanachukuliwa na msisimko bandia, na tunajua kwamba hawana ukweli. . . Ingekuwa heri mbele za Mungu kama wangefanya matengenezo au sivyo waachane na Sabato. Hivyo wasingekuwa kikwazo kwa wasioamini.Mar 157.4

    Mungu hapendezwi na wale ambao wanafanya ulimwengu uwachukie. Kama Mkristo anachukiwa kwa sababu ya matendo yake mema, na kwa kumfuata Kristo, atapata thawabu. Lakini kama anachukiwa kwa sababu yeye mwenyewe anafanya asipendeke, kama anachukiwa kwa sababu ana tabia mbaya, na kwa sababu anaufanya ukweli uwe ni kisa cha ugomvi (au ubishi) kati yake na jirani zake, na kwa sababu amefanya Sabato iwe ni chukizo kwao, basi mtu huyo ni kikwazo kwa wenye dhambi, ni fedheha kwa ukweli mtakatifu, na kama asipotubu, ingekuwa heri kwake kama angefungiwa jiwe la kusagia shingoni, na kisha akatupwa baharini.Mar 157.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents