Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Yesu Alipozaliwa, Sura ya 3

  Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu... mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Mathayo 2:1,2.Mar 11.1

  Mfalme wa amani alishuka chini na kutwaa ubinadamu; na malaika waliokuwa Wameshuhudia utukufu wake katika nyua za mbinguni, alivyokuwa akisujudiwa na jeshi lote la mbinguni, walisikitika walipomwona Jemedari wao wa mbinguni akiwa katika hali duni namna hiyoMar 11.2

  Wayahudi walikuwa wamefarakana na Mungu kwa ajili ya maovu yao kiasi kwamba malaika wasingeweza kuwaletea habari za kuja kwa Mkombozi akiwa kama mtoto mchanga. Mungu aliwachagua Mamajusi wa mashariki kuyatimiza mapenzi yake. . .Mar 11.3

  Mamajusi hawa walikuwa wameona anga likiangazwa na nuru, iliyolifunika jeshi la mbinguni ambalo lilikuwa likiwatangazia wale wachungaji ujio wa Kristo.Mar 11.4

  Nuru hiyo ilikuwa ni kundi la malaika waliokuwa wanang’aa, ambayo ilionekana kama nyota angavu. Mwonekano usio wa kawaida wa nyota hiyo kubwa, ambayo walikuwa hawajawahi kuiona, ikiwa angani kama ishara, ulivuta mawazo yao.... Wale mamajusi walielekea kule nyota ilikokuwa ikiwaongoza. Na walivyokuwa wakiukaribia mji wa Yerusalemu, ile nyota ilionekana kufunikwa na giza, na ikawa haiwaongozi tena. Waliwaza kwamba Wayahudi wasingekosa kujua kuhusu tukio la ujio wa Masihi, na wakawa wanaulizia katika maeneo ya jirani na Yerusalemu.Mar 11.5

  Wale Mamajusi walikuwa wanashangaa kwamba watu walikuwa hawashughuliki na suala la kuja kwa Masihi. . . Wakawa wanashangaa kwamba Wayahudi walikuwa hawajali wala kufurahia matarajio ya tukio kubwa la kuja kwa Kristo.Mar 11.6

  Makanisa ya wakali wetu yanatafuta fahari ya kidunia, na kama walivyokuwa Wayahudi wakati wa ujio wa Kristo mara ya kwanza, hayako tayari kuiona nuru iliyo katika unabii, na kuupokea ushahidi wa kutimia kwa unabii ambao unaonesha kuwa Kristo yu karibu kuja. Wayahudi walikuwa wanatazamia utawala wa kidunia na wenye nguvu katika Yerusalemu. Wakristo wa leo wanategemea mafanikio ya kidunia kwa kanisa, katika kuuongoa ulimwengu, na kufurahia miaka elfu moja ya amani hapa duniani.Mar 11.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents