Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wawakilishi wa Mwokozi, Sura ya 104

    Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa. 1 Petro 2:12.Mar 112.1

    Mungu anategemea ya kwamba wale walichukualo jina la Kristo wamwakilishe Yeye. . . Wanapaswa kutakaswa, kusafishwa, kufa- nywa watakatifu, wakiwasilisha nuru kwa wote wanaokutana nao. . .Mar 112.2

    Wafuasi wa Kristo wanapaswa kujitenga na dunia katika kanuni na matashi yake, lakini hawapaswi kujiweka pembeni na dunia. Mwokozi alijichanganya na watu wakati wote, siyo kwa makusudi ya kuwatia moyo kufanya kinyume na mapenzi ya Mungu, bali kuwainua na kuwaadilisha. “Najiweka wakfu mwenyewe,” alitamka, “Ili na hao watakaswe..” Yn. 17:19. Hivyo Mkristo anapaswa kuishi na watu, ili mwonjo wa upendo wa kimbingu uwe kama chumvi ili kulinda dunia isiharibike...Mar 112.3

    Hitaji letu kuu ni nguvu ya maisha yaliyo ya juu, yaliyo safi, na adiIifu. Ulimwengu unasubiri kuona aina ya matunda yanayotoka kwa Wakristo... Mivuto inayokubaliana na dini ya kibiblia na ile isiyokubaliana nayo, inaendelea kuoeneshwa kwa mawazo ya wote ambao tunapaswa kuwavuta.Mar 112.4

    Mungu na malaika wanatazama. Ni shauku ya Mungu kwamba watu wake waoneshe kwa maisha yao ya kuwa kuna faida katika kuwa Mkristo kuliko kuwa wa dunia, waoneshe kwamba wanatenda kazi katika ngazi iliyo ya juu, tena takatifu. Anatamani kuwaona wakidhihirisha kuwa ukweli ambao wameupokea umewafanya kuwa watoto wa Mfalme wa mbinguni. Anatamani kuwafanya wawe mifereji ambayo kupitia kwayo aweza kumwaga upendo wake usio na kifani na rehema yake.Mar 112.5

    Kristo anasubiri kwa shauku kubwa kudhihirishwa kwake ndani ya kanisa lake. Hapo tabia ya Mwokozi itakapokuwa imenakiliwa ndani ya watu wake, atakuja kuchukua walio wake. Kila Mkristo anayo fursa ya pekee, siyo tu katika kutazamia, bali pia katika kuhimiza ujio wa Bwana wetu. Kama wote wanaojiita kwa jina lake wangezaa tunda kwa ajili ya utukufu wake, mbegu ya injili ingepandwa dunia nzima kwa kasi isiyo ya kawaida! Kwa upesi sana mazao yangekuwa yamekomaa kwa ajili ya mavuno ya mwisho, na Kristo angekuwa amekuja.Mar 112.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents