Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kufundisha Nyumba kwa Nyumba, Sura ya 96

  Ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lolote liwezalo kuwafaa, bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba. Matendo 20:20Mar 104.1

  Washiriki wa makanisa yetu wanapaswa kushughulika zaidi na kazi ya kwenda nyumba kwa nyumba katika kutoa mafundisho ya Biblia na kusambaza vitabu. . .Tunapoendelea kupanda mbegu kila mahali tutatambua ya kwamba “apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.”Mar 104.2

  Kielelezo cha Kristo kinapaswa kufuatwa na wale wanaodai kuwa watoto wake. Ukipunguza mahitaji ya kimwili kwa wanadamu wenzako, utaona ya kwamba shukrani yao itaondoa vizuizi na kukuwezesha kufikia mioyo yao. . . Wanawake kwa wanaume wanaweza kuingia katika kazi hii. . .Wana wa kike wanaweza kufanya kazi ambayo wanaume hawawezi kuifanya katika familia zao, kazi ambayo inafika ndani ya mioyo. Kwa namna hii, wanaweza kukaribia mioyo ambayo wanaume hawawezi kuifikia. Kazi yao inahitajika. Wana wa kike wenye busara na wanyenyekevu wanaweza kufanya kazi nzuri katika kuueleza ukweli kwa watu katika nyumba zao. Neno la Mungu likiwa limeelezwa hivi litaweka chachu katika kazi, na. . . familia nzima zitaongoka.Mar 104.3

  Katika mkao wa familia nyumbani, barazani mwa jirani yako, kando kando ya kitanda alimo mgonjwa, kwa namna iliyo tulivu waweza kusoma Maandiko na kunena neno la Yesu na kweli yake. Mbegu ya thamani yaweza kupandwa kwa namna hiyo na matokeo yake itaota na kukua na kisha kuzaa matunda...Mar 104.4

  Ipo kazi ya kimishenari ya kufanywa katika maeneo mengi yaonekanayo kutotoa matumaini. Roho ya kiinjilisti inahitajika ili itawale roho zetu, na kutuvuvia uwezo wa kufikia viwango vya watu ambao hatukupanga kuwafanyia kazi na katika njia na mahali ambapo hatukuwaza kuwa tungepafanyia kazi. Bwana anao mpango wake kwa ajili ya kupanda mbegu ya injili. Kulingana na mapenzi yake, tunapopanda mbegu, tutazidisha kiasi kwamba neno lake Iitawafikia maelfu ambao kamwe hawajapata sikia ukweli.Mar 104.5

  Maefu kwa maelfu, na makumi elfu kwa makumi elfu ya malaika wanasubiri kushirikiana na washiriki wa makanisa yetu katika kuwasiliana na wengine nuru ambayo Mungu ametupatia kwa ukarimu, ili watu waandaliwe kwa ajili ya ujio wa Kristo.Mar 104.6

  Dada zetu, vijana, watu wenye rika la kati, na walio wazee, wanaweza kufanya sehemu yao katika kazi ya kuhitimisha wakati huu; na kadiri wapatapo nafasi na kutenda hili, wao wenyewe watapokea uzoefu wenye thamani kubwa. Wanapoendelea kusahau nafsi zao, wataendelea kukua katika neema.Mar 104.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents