Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Dunia Katika Uhitaji, Sura ya 95

  Twatazamia nuru, na kumbe! Latokea giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu. Isaya 59:9Mar 103.1

  Wapo wengi ambao hata ingawa wanasoma Maandiko, hawaelewi yanachokimaanisha hasa. Duniani kote, watu wanatazama mbinguni kwa shauku kubwa. Sala, machozi na maswali yanayotoka katika roho za watu yanatamani nuru, neema, na Roho Mtakatifu. Wengi wamo katika ukingo wa ufalme, wakisubiri kukusanywa.Mar 103.2

  Kila mahali kuna mioyo iliayo kwa ajili ya kile wanachokihitaji. Wanatamani uwezo utakaowapa ushindi dhidi ya dhambi, nguvu itakayowakomboa toka katika utumwa wa uovu, uwezo ambao utawapa afya, uhai na amani. Wengi ambao waliwahi kujua nguvu ya neno la Mungu, wamedumu kuwa mahali ambapo Mungu haheshimiki, na sasa wanautamani uwepo wa uungu.Mar 103.3

  Leo, dunia mahitaji kile ilichokihitaji takriban miaka elfu mbili iliyopita - ufunuo wa Kristo. Kazi kuu ya matengenezo inahitajika, na ni kwa neema ya Kristo tu kazi ya urejeshwaji, kimwili, kiakili na kiroho inaweza kukamilishwa.Mar 103.4

  Mbinu ya Kristo peke yake ndiyo iwezayo kuleta mafanikio katika kuwafikia watu. Mwokozi alichangamana na watu kwa namna iliyoonesha kupenda mafanikio yao. Aliwahurumia, aIijishughuIisha na mahitaji yao, na alipata kibali kwao. Kisha akawaalika akisema, “Nifuateni.”Mar 103.5

  Kuna hitaji la kufanya juhudi binafsi ili kuwa karibu na watu... Tunapaswa kulia nao waliao, na kufurahi pamoja nao wanaofurahi. Hali tukiwa na uwezo wa kushawishi, nguvu ya maombi na nguvu ya upendo wa Mungu, kazi hii haitakuwa ya bure.Mar 103.6

  Nguvu za kimbingu zinasubiri kuungana katika ushirika na nguvu za kibinadamu, ili kuufunulia ulimwengu kile ambacho wanadamu wanaweza kuwa, na kile ambacho kutokana na muunganiko huu, kinaweza kufanyika kwa ajili ya kuokoa roho zinazopotea. Utumishi wa mtu ambaye ameikana nafsi na kutoa moyo wake kwa ajili ya kazi ya Roho Mtakatifu na kuishi maisha yaliyotolewa kikamilifu kwa Mungu, una faida isiyo kifani.Mar 103.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents