Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ahadi ya Mungu Kuhusu Usalama, Sura ya 88

    Basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu. 2 Petro 2:9.Mar 96.1

    Wakati wa jaribio lililo mbele yetu ahadi ya Mungu ya usalama itawekwa kwa ajili ya wale ambao wameishika subira yake... Nguzo ya wingu ambayo uwepo wake unatamka ghadhabu na utisho kwa waasi wa sheria ya Mungu ni nuru na rehema na ukombozi kwa wale ambao Wameshika amri zake. Mkono ulio na nguvu ya kupiga waasi utakuwa na nguvu ya kuwakomboa walio watii. Kila aliye mwaminifu ni hakika kwamba atakusanywa....Mar 96.2

    Utafanya nini wakati wa matukio ya kufungwa kwa historia ya dunia?... Je, unatambua kazi kuu ya maandalizi ambayo inaendelea mbinguni na duniani? Hebu yeyote asicheze na dhambi, ambacho ni chanzo cha kila namna ya unyonge duniani... Usiache hatima ya roho yako isiwe na uhakika. Unapaswa kujua kama uko kikamilifu upande wa Bwana. Hebu maswali na yatoke katika mioyo na midomo yenye kutetema, “Ni nani awezaye kusimama?” Je, katika muda huu wa thamani wa rehema, mmekuwa mkihifadhi nyenzo muhimu kwa ajili ya ujenzi wa tabia? Je, mmekuwa mkisafisha madoa yote katika roho zenu? Je, mmeifuata nuru? Je, matendo yenu yameambatana na imani mnayo dai kuwa nayo?Mar 96.3

    Je, mvuto unaonyenyekeza na kulainisha wa neema ya Mungu linafanya kazi ndani yako?...Je, nuru yako inang’aa ili kuwaangazia mataifa ambao wanaangamia katika dhambi zao? Je, unatambua ya kwamba unapaswa kusimama ukitetea amri za Mungu mbele za wale wanaozikanyaga?Mar 96.4

    Inawezekana kuwa muumini wa kawaida, asiye na kina katika imani, na matokeo yake kuonekana umepungua na kupoteza uzima wa milele. Inawezekana kabisa ukawa mtendaji wa matakwa ya Biblia na kufikirika kuwa Mkristo, na bado ukaangamia kwa sababu ya upungufu wa sifa muhimu za tabia ya Kikristo.... Na tufanye kazi makini kwa ajili ya umilele hali rehema ikiendelea kuwepo, na Mwokozi akiendelea kufanya upatanisho.Mar 96.5

    Zahama kuu iko mbele yetu. Ili kukabili majaribio yake, na kukamilisha majukumu yetu, kunahitajika imani inayodumu. Lakini twaweza kufanikiwa kwa utukufu; roho yoyote ikeshayo, inayosali, inayoamini haitanaswa na adui.Mar 96.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents