Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wazo Kuu la Maandiko, Sura ya 5

    Lakini mimi najua ya kuwa mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Ayubu 19: 25Mar 13.1

    Ukweli mmoja muhimu na wenye utukufu unaoonekana katika maandiko ni ule wa kuja kwa Yesu mara ya pili; ili kukamilisha kazi kubwa ya ukombozi. Katika ahadi ya kuja kwake, yeye ambaye ni ufufuo na uzima, akija kuwaleta nyumbani wale waliokuwa wametengwa, tumaini la kutia moyo linatolewa kwa wasafiri wa Mungu, walioachwa muda mrefu wakikaa “katika nchi na uvuli wa mauti.” Fundisho la kuja kwa Yesu mara ya pili ni wazo kuu la Maandiko Matakatifu. Tangu siku ile wale wanandoa wa kwanza walipogeuza hatua zao kwa huzuni na kutoka katika Bustani ya Edeni, watoto wa imani wamekuwa wakisubiri kuja kwa yule aliyeahidiwa, kuivunja nguvu ya yule mharibifu na kuwarudisha katika Paradiso iliyokuwa imepotea. ....Henoko, aliyekuwa wa saba tu kutoka kwa wale waliokuwa wakiishi katika bustani ya Edeni, ambaye alitembea na Mungu kwa karne tatu hapa duniani, aliwezeshwa kuuona ujio wa Mkombozi kwa mbali. Alisema, “Angalia Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, ili afanye hukumu juu ya watu wote.” Mzee Ayubu katika kipindi kigumu cha mateso yake alisema kwa imani thabiti, “Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi: ....lakini katika mwili wangu nitamwona Mungu. Nami nitamwona mimi nafsi yangu, na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine.”Mar 13.2

    Mungu wa neema yote na awape ufahamu ili mweze kuyaona mambo ya milele, ili mweze kuyaona makosa yenu, ambayo ni mengi, kama yalivyo, ili mfanye juhudi zinazohitajika kuyaondoa, na pale palipo na tunda hili ovu, mzae matunda yaliyo na thamani hata kuwafikisha katika uzima wa milele.Mar 13.3

    Inyenyekezeni mbele za Mungu mioyo yenu iliyo duni na yenye kiburi na kujihesabia haki; jishusheni sana, tena sana, chini ya miguu yake, mkiwa mmepondeka katika hali yenu ya dhambi. Tumia muda, nguvu na akili zako zote katika kazi ya kujiandaa. Usiache hadi utakapoweza kusema: Mkombozi wangu yu hai, na kwa kuwa yu hai, mimi pia nitakuwa hai.Mar 13.4

    Ukikosa kuingia mbinguni, utakuwa umekosa kila kitu; ukiingia mbinguni, utakuwa umepata kila kitu. Nakusihi, usije ukafanya makosa katika jambo hili. Jambo hili linahusu faida ya milele.Mar 13.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents