Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Majaribu Yaliyofichwa, Sura ya 52

    Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. Matendo 20:29,30Mar 60.1

    Mungu hajawaruka watu wake na kuchagua mtu mmoja hapa na mwingine pale kama watu wafaao kukabidhiwa ukweli. Mungu hampatii mtu mmoja nuru mpya kinyume na imani aliyoiimarisha katika kanisa. Katika kila mwamko wa matengenezo, wapo ambao wameinuka wakidai hivyo. . .Mar 60.2

    Mtu mmoja anakubali dhana mpya na yenye asili ambayo haionekani kupingana na kweli. Anadumu katika dhana hii hadi inapoonekana kwake kuwa imevikwa uzuri na umuhimu, kwani Shetani anao uwezo wa kuweka mwonekano huo usio wa kweli. Hatimaye, inakuwa ni mada inayoteka mawazo kabisa, linakuwa jambo kuu ambalo linakuwa kiini cha mawazo yote; matokeo yake kweli inang’olewa toka moyoni. . .Mar 60.3

    Ninawaonyeni kuweni makini dhidi ya masuala kama haya, ambayo yamekusudiwa kugeuza mawazo toka katika kweli. Hakuna makosa yasiyo na madhara. Kamwe makosa hayatakasi, bali daima huleta machafuko na mfarakano. . .Mar 60.4

    Yapo majaribu elfu ambayo yamefichwa huku yakiwa yameandaliwa kwa ajili ya wale walio na nuru inayotokana na kweli; na usalama pekee kwa yeyote kati yetu upo katika kutopokea fundisho lolote jipya, ufasiri mpya wa Maandiko, bila kuukabidhi kwanza kwa ndugu wenye uzoefu. Weka fundisho hilo mbele yao kwa unyenyekevu, roho inayofundishika na pia sala ya dhati; na kama hawaoni nuru katika hili, liache na kubali ushauri wao. . .Mar 60.5

    Shetani yuko kazini siku zote; lakini ni wachache wajuao hata kwa kiasi kidogo tu anavyoshughulika na mbinu zake tatanishi. Sharti watu wa Mungu wajiandae kusimama imara dhidi ya huyu adui mjanja. Huu ndiyo upinzani ambao Shetani anauogopa. Anajua vema zaidi ya jinsi tunavyojua na uwezo wake na jinsi anavyoweza kushindwa kwa urahisi kama tukimpinga na kumkabili moja kwa moja. Kwa kutumia uwezo wa kimbingu, mtakatifu aliye dhaifu sana anakuwa na nguvu sana kumzidi Shetani na malaika zake, na kama akiwekwa katika jaribio anaweza kuthibitisha uwezo wake ulio bora zaidi ya ule wa mwovu. Kwa sababu hiyo, hatua za Shetani huwa za kimya kimya, akitembea kwa kunyata, na silaha zake zikiwa zimefichwa. Hadiriki kujionesha kwa uwazi, kwani kwa kufanya hivyo atashtua uwezo wa Mkristo uliolala ambao unampeleka kwa Mungu kwa njia ya sala.Mar 60.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents