Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kichwa cha Nyumba Kumwiga Kristo

    Mkuu wa watu wote nyumbani ni baba. Yeye ndiye mwenye kutunga sheria, na kuonyesha kwa kielelezo chake mwenyewe cha kiume kwamba anazo tabia thabiti; nguvu, uaminifu, unyofu, uvumilivu, moyo mkuu, bidii, na hali ya manufaa. Baba kwa neno moja ni kuhani wa watu wa nyumbani, awekaye madhabahuni mwa Mungu dhabihu ya asubuhi na jioni. Mke na watoto wangetiwa moyo kujiunga katika kuitoa sadaka hii na pia kushiriki wimbo wa kumsifu Mungu. Asubuhi na jioni, baba kama kuhani wa watu nyumbani, angeungama mbele za Mungu dhambi alizotenda yeye mwenyewe na zile walizotenda watoto wake katika siku hiyo. Dhambi zile azijuazo na zile za siri pia ambazo jicho lake Mungu peke yake limeziona; zote yapasa ziungamwe. Kanuni hii, ikitimizwa kwa moyo wa bidii na baba wakati akiwapo au na mama wakati baba asipokuwapo nyumbani itawaletea mibaraka watu wa nyumbani.KN 165.5

    Kwa mwanaume ambaye ndiye mume na baba, napenda kusema, Hakikisha kwamba tabia safi, takatifu zaizunguka roho yako. Yakupasa kujifunza kila habari za Kristo. Kamwe haikupasi kuonyesha moyo wa udhalimu nyumbani. Mtu afanyaye hivi anatenda kazi pamoja na malaika wabaya. Yaweke mapenzi yako chini ya mapenzi ya Mungu. Fanya yote uwezayo kuyafanya maisha ya mkeo yawe mazuri na ya raha. Litwae Neno la Mungu liwe mshauri wako. Nyumbani yashike mafundisho ya Neno la Mungu. Ndipo utayashika maishani mwako kanisani nawe utaweza kulichukua manali unapofanyia kazi yako. Kanuni za mbinguni zitakuwezesha yote utendayo. Malaika wa Mungu watashirikiana nawe, wakikusaidia kumdhihirisha Kristo kwa walimwengu. Usikubali masumbuko ya kazi yako kuleta giza kwenye maisha yenu nyumbani. Kama, wakati mambo madogo madogo yanapotokea ambayo si sawa, unashindwa kuwa na saburi, uvumilivu, moyo wa fadhili, na upendo, hilo huonyesha kwamba hujamchagua kama rafiki yako Yeye ambaye alikupenda hata akautoa uhai wake kwa ajili yako, kusudi upate kuwa na umoja nave.KN 166.1

    Ni jambo lionyeshalo tabia ya kiume aliyo nayo mume akifikiri daima cheo chake kama kichwa cha jamaa. Haimwongezei heshima kumsikia akiyatumia maneno ya Biblia kusaidia madai yake na madaraka yake. Haitamfanya azidi kuwa hodari kumtaka mkewe, mama na watoto wake, kutekeleza mipango ya mumewe kana kwamba haiwezi kukosewa. Bwana amemweka mume kichwa cha mke awe mlinzi wake; yeye ndiye kiungo cha jamaa, akiwafunga pamoja watu wa nyumbani, kama Kristo alivyo kichwa cha Ramsa na Mwokozi wa mwili. Hebu kila mume anayedai kumpenda Mungu ajifunze kwa uangalifu mapenzi ya Mungu katika cheo chake. Mamlaka ya Kristo yametumiwa kwa busara, kwa wema na upole wote; basi mume na autumie uwezo wake na kumwiga Kichwa kikuu cha kanisa. 3AH 212-215;KN 166.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents