Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 5 - Kristo Haki Yetu

    “TUKIZIUNGAMA dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9).KN 54.1

    Mungu anataka tuziungame dhambi zetu, na kunyenyekea kumtumaini kama baba mwenye upendo ambaye hatawatupa wale ambao wanamtumainia. Wengi wetu tunaenenda kwa kuona kwa macho, wala siyo kwa imani. Tunayaamini mambo yale tuyaonayo, lakini hatuzithamini ahadi za thamani tulizopewa katika neno la Mungu; lakini hatuwezi kumwaibisha Mungu kwa makusudi zaidi ya kuonyesha kwamba hatuamini asemalo, na kuuliza kama Mungu ni mwaminifu kwetu sisi au anatudanganya.KN 54.2

    Mungu hatuachi kwa sababu ya dhambi zetu. Pengine tunaweza kufanya makosa, na kumhuzunisha Roho wake; lakini tukitubu, na kumwendea kwa mioyo yenye toba, hatatufukuza. Viko vipingamizi vipaswavyo kuondolewa. Moyo mbaya umekuwapo, na pamekuwapo na kiburi, majivuno, kutosubiri, na manung’uniko. Haya yote hututenga na Mungu. Dhambi hazina budi kuungamwa, yapasa pawepo kazi kubwa yenye kina ya neema moyoni. Wale wanaojiona dhaifu na waliokata tamaa waweza kuwa watu wa Mungu wenye nguvu, na kufanya kazi bora kwa Bwana. Lakini hawana budi kufanya kazi kutoka kwa fikra za juu; hawana budi kuepukana na mvuto wa nia ya kujifikiri nafsi mwenyewe bila kujali wengine.KN 54.3

    Yatupasa kujifunza katika shule ya Kristo. Hakuna kitu kingine ila haki yake tu ambayo ndiyo iwezayo kutupa haki ya mmojawapo wa mibaraka ya agano la neema. Tumetamani kwa muda mrefu na kujaribu kuipata mibaraka hii, lakini hatukuipokea, kwa sababu tumependelea wazo kwamba tungeweza kufanya kitu kutustahilisha mibaraka hiyo. Hatukuacha kujitazama wenyewe, na kuamini kuwa Yesu ni Mwokozi aliye hai. Haitupasi kufikiri kuwa neema yetu wenyewe na sifa zetu njema zitatuokoa; neema ya Kristo ndilo tu tumaini letu la wokovu. Kwa njia ya nabii wake Bwana anaahidi, “Mtu mbaya na aache njia yake na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie Bwana, naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa” (Isaya 55:7). Yatupasa kuiamini ahadi kama ilivyo, wala siyo kukubali maoni ya moyoni kwa imani. Tukimwamini Mungu kabisa, tunapotegemea juu ya sifa njema za Yesu kama Mwokozi mwenye kusamehe dhambi, tutapokea msaada wote tutakaouhitaji. Tunajitazama nafsi, kana kwamba tunaweza kujiokoa nafsi zetu wenyewe; lakini Yesu alitufilia kwa sababu sisi wenyewe hatuwezi kujiokoa. Tumaini letu , pamoja na haki yetu viko kwake. Hatupaswi kukata tamaa, na kuogopa kwamba hatuna wa kutuokoa, au kwamba hakusudii kuturehemu. Wakati huu anapoendesha kazi yake kwa ajili yetu, anatualika kumwendea katika hali yetu dhaifu, bila msaada, tukaokolewe. Tunamtweza kwa kutokuamini kwetu. Ni jambo la kushangaza jinsi tunavyomtendea huyu Rafiki yetu mkubwa, jinsi tumaini letu lilivyo kidogo kwake yeye ambaye aweza kutuokoa kabisa, na ambaye ametupa kila jambo lionyeshalo upendo wake mkuu.KN 54.4

    Ndugu zangu, mnatazamia kuwa tabia yenu nzuri itawashuhudia mpate kibali kwa Mungu, mkifikiri kuwa kwanza hamna budi kuachana na dhambi kabla ya kuuamini uwezo wake wa kuokoa? Kama haya ndiyo mashindano yanayoendelea mioyoni mwenu, hamtapata nguvu, na mwishowe mtakata tamaa.KN 55.1

    Jangwani, wakati Bwana alipowaruhusu nyoka wenye sumu kuwauma Waisraeli walioasi, Musa aliagizwa kuinua nyoka wa shaba nyeupe, na kuwaamuru wote waliojeruhiwa kumwangalia ili wapate kupona. Lakini wengi hawakuona msaada katika dawa hii iliyoamriwa na Mungu. Maiti na watu waliokuwa katika hali ya kufa waliwazunguka pande zote, nao wakajua kuwa pasipo msaada wa Mungu hakika watakufa; lakini walilia na kuomboleza kwa sababu ya majeraha yao, maumivu yao, mauti yao mpaka wameishiwa na nguvu zao, na macho yao yamegeuka kama ya mtu kifoni, wakati ambapo wangeweza kuponywa mara moja kama wangemtazama yule nyoka.KN 55.2

    “Kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika Yeye.” Kama unafahamu dhambi zako, usizitumie nguvu zako zote kuomboleza juu yake, bali tazama upate kuponywa. Yesu ndiye Mwokozi wetu peke yake; na ijapokuwa mamilioni wenye kuhitaji kuponywa watakataa rehema yake iliyotolewa, hakuna mtu ambaye ataamini sifa njema za Kristo atakayeachwa apotee. Kwa kuwa tunajua kwamba bila Kristo maishani tu wadhaifu sana, haitupasi kukata tamaa; inatupasa kumtegemea Mwokozi aliyesulibiwa na kufufuka. Jipe moyo maskini, mgonjwa wa dhambi, ulioyekata tamaa, tazama upate kuponywa. Yesu ameahidi katika neno lake ya kuwa atawaokoa wote wanaomwendea.KN 55.3

    Njoo kwa Yesu, na upate pumziko na amani. Unaweza kupata mbaraka hata sasa. Shetani anakushauri kuwa u mdhaifu, bila msaada, na huwezi kujibariki mwenyewe. Ni kweli; u mdhaifu. Lakini mwinue Yesu mbele ya Shetani: “Ninaye Mwokozi aliyefufuka katika wafu. Namwamini, hataniacha nishindwe. Katika jina lake nitashinda. Ndiye haki yangu, na taji iletayo shangwe.” Pasiwepo mtu hata mmoja hapa anayeona moyoni kuwa hali yake haina matumaini; kwa kuwa sivyo ilivyo. Waweza kuona kwamba u mwenye dhambi na mpotevu; lakini hii ndiyo sababu unahitaji Mwokozi. Kama unazo dhambi za kuungama, usipoteze wakati. Dakika hizi ni za thamani kuu. “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9). Wale wenye njaa na kiu ya haki watajazwa; maana Yesu ameahidi hilo. Mwokozi wa ajabu! Mikono yake imekunjuliwa kutupokea, na moyo wake mkuu wa upendo unangojea kutubariki.KN 56.1

    Wengine huelekea kuona moyoni kwamba hawana budi kuangaliwa waonekane kama wanafaa au hawafai, na ya kuwa hawana budi kuthibitisha kwa Bwana kuwa wameongoka, kabla hawajaweza kudai mbaraka wake. Lakini watu hawa wa thamani wanaweza kuudai mbaraka wake hata sasa. Yawapasa wapate neema yake, Roho wa Kristo, atakayewasaidia katika udhaifu wao, ama sivyo hawawezi kukuza tabia ya Kikristo. Yesu anapenda tumwendee, hivi tulivyo-wenye dhambi, wadhaifu, wasiojitegemea.KN 56.2

    Toba, na msamaha pia, ni vipawa vya Mungu kwa njia ya Kristo. Ni kwa njia ya mvuto wa Roho Mtakatifu tunawezeshwa kuona hatia ya dhambi, na kuiona haja yetu ya msamaha. Wenye masikitiko kwa ajili ya makosa yao, na wala si wengine, ndio wanaosamehewa; lakini neema ya Mungu ndiyo inayoufanya moyo utubu. Anajua udhaifu wetu wote na upungufu, naye atatusaidia.KN 56.3

    Wengine wanaomwendea Mungu kwa kutubu na kuungama na hata kuamini kuwa dhambi zao zimesamehewa, wangali wanakosa kudai, kama wapaswavyo, ahadi za Mungu. Hawaoni kuwa Yesu ni Mwokozi aliyehai daima; nao hawako tayari kukabidhi roho zao kwake azilinde na kumtegemea kuikamilisha kazi ya neema iliyoanzwa mioyoni mwao. Huku wakidhani wanajikabidhi kwa Mungu, wanajitegemea nafsi wenyewe zaidi. Ni wenye bidii wanaomwamini Mungu kwa sehemu na kwa sehemu kujiamini wenyewe. Hawamwangalii Mungu, kuwekewa uwezo wake, bali hutegemea kujihadhari na vishawishi, na kutenda wajibu fulani ili awakubaliwa. Hakuna ushindi katika imani ya namna hii. Watu wa jinsi hii husumbuka bure, bila kuwa na kusudi; roho zao daima ziko kifungoni, nao hawatapata pumziko hadi watakapoweka mizigo yao miguuni pa Yesu.KN 56.4

    Kuna haja ya uangalifu wa daima, uaminifu, na uchaji wa upendo; lakini mambo haya yatakuja yenyewe wakati moyo wa mtu unapowekewa uwezo wa Mungu kwa njia ya imani. Hatuwezi kufanya lo lote, hata kidogo, kujistahilisha kupata kibali cha Mungu. Haitupasi kujitegemea hata kidogo wala kuyategemea matendo yetu mema; lakini kama wakosaji, wenye dhambi tukimwendea Kristo, twaweza kupata pumziko katika pendo lake. Mungu atampokea kila mmoja amwendeaye akiamini kabisa sifa njema za Mwokozi aliyesulibishwa. Upendo hutokea moyoni. Pengine hapawezi kuwapo kipindi cha kuona furaha moyoni, lakini kuna tumaini lidumulo la amani. Kila mzigo ni mwepesi. Kazi inakuwa furaha, na dhabihu jambo la kupendeza. Njia ambayo zamani ilionekana kama ilifunikwa gizani huwa safi ing’aayo kwa mionzi ya nuru itokayo kwa Jua la Haki. Huku ndiko kuenenda katika nuru kama Kristo alivyo katikanuru. 1(2 TT 91-95)KN 57.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents