Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Zipimeni Shuhuda Hizi kwa Matunda Yake

    Hebu Shuhuda hizi zipimwe kwa matunda yake. Roho ya mafundisho yake ni nini? Matokeo yake ya baadaye ya mvuto wao ni nini? Wote wanaotaka sana kufanya hivyo wanaweza kufahamu vizuri matunda ya niozi hizi. Mungu ameona yafaa kufahamu vizuri matunda ya njozi hizi. Mungu ameona yafaa kuwaacha wazidi kukaa na kuimarika katika kushindana na nguvu za Shetani na mvuto wa wanadamu ambao wamemsaidia Shetani kazini mwake.KN 107.3

    Ama Mungu analifundisha kanisa lake, akigombeza makosa yao na kuimarisha imani yao, ama sivyo. Kazi hii ama ni ya Mungu, ama sivyo. Mungu hashirikiani na Shetani kwa lo lote. Kazi yangu .... ama ni yenye muhuri ya Mungu ama muhuri ya yule adui. Hakuna kazi nusu nusu katika neno hili. Shuhuda hizi ama ni za Roho wa Mungu, ama wa Ibilisi.KN 107.4

    Kama Mungu alivyojidhihirisha kwa njia ya Roho ya unabii, wakati uliopita, wakati uliopo, na wakati ujao umepita mbele yangu. Nimeonyesnwa nyuso ambazo kamwe nalikuwa sijaziona, na miaka ya baadaye nalizitambua nilipoziona. Naliamshwa usingizini nikijua dhahiri mafundisho niliyoonyeshwa akilini mwangu; nami nimeandika usiku wa manane, barua ambazo zimekwenda hata kulivuka bara hili na, zikikutana na wakati wa hatari, zimeepusha hasara kubwa kwa kazi ya Mungu. Hii imekuwa ndiyo kazi yangu kwa miaka mingi. Nimetiwa nguvu kukaripia na kugombeza makosa ambayo nalikuwa sikuyafikiri. Je, kazi hii yatoka juu au yatoka chini? 55T 671;KN 107.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents