Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuwaacha Watoto Kukua Ujingani ni Dhambi

    Wazazi wengine wameshindwa kuwapa watoto wao mafundisho ya dini, na hawakujali pia elimu yao ya shuleni. Si vizuri kukosa kujali hata mojawapo ya mambo hayo. Akili za watoto zitakuwa nyepesi, na kama hazijishughulishi kwa kazi za nje, au kushikwa na masomo, zitahatarishwa kwa mivuto mibaya. Ni dhambi kwa wazazi kuwaacha watoto wao kukua ujingani. Yawapasa kuwapatia vitabu vizuri vya manufaa, na wangewafundisha kufanya kazi, kuwa na saa za kazi ya juhudi, na saa za kutumia kwa kujifunza na kusoma. Wazazi wangefanya bidii kuadilisha mioyo ya watoto wao na kuzidisha ubora wa akili zao za kichwani. Akili isipotumiwa, bila kukuzwa kwa kawaida huwa pungufu, ya ufisadi, na mbovu. Shetani hutumia vizuri nafasi yake na kukuza na kuongoza akili za watu wavivu. 121T 398, 399KN 219.1

    Kazi ya mama huanza mtoto akiwa mchanga bado. Yampasa kutuliza nia na hasira ya mtoto wake, na kumtiisha, kumfundisha kutii. Mtoto akizidi kukua, usilegeze mkono. Yafaa kila mama kutwaa wasaa kushauriana na watoto wake, kuwatoa makosa yao, na kuwafundisha kwa uvumilivu njia iliyo bora. Wazazi walio Wakristo wangejua kuwa wanawafundisha na kufanya watoto wao kufaa kuwa watoto wa Mungu. Mambo yote ya maisha ya dini ya watoto hao huongozwa na mafundisho yanayotolewa, na tabia inayofanyizwa na nia ya wazazi, itakuwa shida kujifunza fundisho miaka ya baadaye. Mashindano makali kama nini, vita kali kama nini, kujaribu kuishinda ile nia ambayo kamwe haikulainishwa, ipate kuyatii mapenzi ya Mungu! Wazazi wasiojali kazi hiyo kubwa hufanya kosa kuu, na kutenda dhambi kwa watoto wao maskini na kwa Mungu pia. 131T 390, 391;KN 219.2

    Wazazi, mkikosa kuwapa watoto wenu elimu ambayo Mungu ameifanya wajibu wenu kuwapa, itawabidi kumjibu kwa ajili ya matokeo ya baadaye. Matokeo hayo hayataonekana kwa watoto wenu tu. Kama vile mbaruti mmoja ukiachwa kuota shambani unavyozaa mavuno ya namna yake, kadhalika ndivyo dhambi zinazotokana na uzembe wenu zitakavyofanya kazi kuwaharibu wote wanaokutana na mvuto wao. 14CG 115;KN 219.3

    Laana ya Mungu kwa hakika itawakalia wazazi wasio waaminifu. Licha ya kupanda miiba ambayo itawajeruhi hapa, hata itawabidi kukutana na matokeo ya kukosa kwao uaminifu wakati hukumu itakapokaa. Watoto wengi watainuka hukumuni na kuwashtaki wazazi wao kwa kutowazuia, na kuwashtaki juu ya maangamizo yao. Huruma za bure na upendo wa kijinga wa wazazi huwafanya kuyasamehe makosa ya watoto wao na kuyapita bila kuwarudi, na natimaye watoto wao hupotea, na damu ya roho zao itawakalia wazazi wasio waaminifu. 151T 219;KN 219.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents