Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 23 - Mama na Mtoto Wake

    BADALA ya kuzama kwenye kazi ya kuchosha ya watu wa nyumbani, hebu mke yaani mama atwae wasaa kusoma, kujielimisha, kuwa rafiki wa mumewe, na kujua maendeleo ya akili za moyoni za watoto wake. Hebu atumie kwa busara nafasi aliyo nayo sasa kuwavuta wapenzi wake kwa ajili ya maisha bora zaidi. Na atwae nafasi kumfanya Mwokozi mpendwa kuwa Rafiki wa daima na Msiri mkuu. Na atwae wasaa kwa kusoma Neno la Mungu, na kwenda pamoja na watoto mashambani na kujifunza habari za Mungu kwa njia ya kuutazama uzuri wa kazi zake Mungu.KN 157.1

    Hebu awe mchangamfu na mwenye furaha. Badala ya kutumia kila dakika katika kushona kusiko na mwisho, na ufanye wakati wa jioni kuwa saa nzuri ya kustarehe, ya watu wa nyumbani kukutana tena pamoja baada ya kazi za mchana kutwa. Kwa njia hii watu wengi wangeweza kuongozwa kuipendelea jamaa hii kabla hawajachagua klabu ya pombe, Wavulana wangezuiwa wasiende mabarabarani. Wasichana wengi wangeepushwa na marafiki wasio na maana, wanaopoteza. Mvuto wa nyumbani ungekuwa kwa wazazi na watoto kile Mungu alichokusudia, kuwa mbaraka siku zote za maisha.KN 157.2

    Swali liulizwalo mara kwa mara ni, “Mke asiwe na uhuru kuchagua apendavyo mwenyewe?” Biblia yaeleza wazi kuwa mume ni kichwa cha watu wa nyumbani. “Enyi wake, watiini waume zenu.” Kama agizo hili lingeishia hapa, tungeweza kusema kuwa cheo cha mke si cha kutamanika; lakini, tusome mwisho wa agizo hilo hilo, yaani, “kama kumtii Bwana wetu.”KN 157.3

    Yatupasa kuwa na Roho wa Mungu, ama sivyo hatuwezi kuwa na masikilizano nyumbani. Mke, kama akiwa na Roho wa Kristo, atajihadhari na maneno yake; ataitawala roho yake, na kuwa mtiifu, wala hataona kuwa ni mtumwa, bali rafiki kwa mumewe. Kama mume ni mtumishi wa Mungu, hatajifanya bwana kwa mkewe; hatakuwa mdhalimu, asiyeshauriana na mtu juu ya neno lo lote, na mkali. Hatuwezi kufurahia upendano wa nyumbani kama tukiwa na wasiwasi mwingi; maana nyumbani, Roho wa Mungu akikaa humo, panafanana na mbinguni. Ikiwa mmoja anafanya kosa, mwingine atumie uvumilivu kama ule wa Kristo, wala asikate tamaa. 1AH 110-118;KN 157.4

    Kila mwanamke aliye karibu kuwa mama, ijapokuwa mazingira yake yawe ya namna gani, daima angetia moyo mambo ya kufurahisha, uchangamfu, tabia thabiti, akijua kuwa kujitahidi kwake katika jambo hili kutalipwa mara kumi katika mwili, na katika tabia ya adili ya mtoto wake. Wala si hivyo tu. Aweza kuzoea kufikiri mambo mazuri ya kumpendeza, na kwa kufanya hivyo kuudumisha moyo wa furaha mawazoni na kueneza uchangamfu na furaha yake mwenyewe kwa watu wa nyumbani mwake, na kwa wale wanaoshirikiana naye. Kwa kiasi kikubwa afya yake itafanywa kuwa bora zaidi. Nguvu itatolewa kwa chemchemi za uzima, damu itatembea vizuri, siyo pole pole, kama ingalivyofanya ikiwa angekubali kufa moyo na kuhuzunika. Hali yake njema ya akili na ya tabia ya moyoni hutiwa nguvu na moyo wake wa ukunjufu. Uwezo wa nia huweza kupinga maneno ya moyoni nao utakuwa kitulizo kikubwa cha mishipa ya fahamu. Watoto wanaonyang’anywa nguvu hiyo ambayo wangepaswa kuirithi kutoka kwa wazazi wao wangeangaliwa sana. Kwa kuziangalia sana kanuni za mwili wao hali lliyo nzuri zaidi ya mambo huweza kuanzishwa.KN 157.5

    Mwenye kutazamia kuwa mama angeitunza roho yake katika upendo wa Mungu. Moyo wake wapaswa uwe na amani; angepata raha katika upendo wa Yesu, akiyatimiza maneno ya Knsto. Angekumbuka kuwa mama ni mtenda kazi pamoja na Mungu.KN 158.1

    Mume na mke wanapaswa kushirikiana. Tungekuwa na ulimwengu mzuri namna gani kama akina mama wote wangejitoa wakfu kwa Mungu na kumtoa wakfu mtoto wao, kabla ya na baada ya kuzaliwa kwaKe!KN 158.2

    Matokeo ya baadaye ya mivuto kabla ya kuzaa kudharauliwa na wazazi wengi kama jambo lisilo na maana; lakini mbinguni sivyo inavyohesabiwa. Ujumbe uliotumwa kwa njia ya malaika wa Mungu, na kutolewa mara mbili kwa njia nzito sana, huonyesha kwamba jambo hili linapasa tulifikiri sana.KN 158.3

    Maneno aliyoambiwa mama Mwebrania (mkewe Manoa), Mungu huwaambia mama wote wa kila kizazi. Malaika asema, “Asile kitu cho chote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze.” Hali njema ya mtoto itadhuriwa na mazoea mabaya ya mama. Tamaa zake za chakula na tamaa mbaya za mwili hazina budi kutawaliwa na kanuni inayoyaongoza maisha. Yako mambo apaswayo kuepukana nayo, mambo apaswayo kuyapinga, kama akitaka kulitimiza kusudi la Mungu kwake katika kumpa mtoto aliye naye.KN 158.4

    Ulimwengu umejaa mitego waliyowekewa vijana. Watu wengi huvutwa macho na maisha ya choyo, ama moyo wa kujipendeza nafsi mwenyewe na anasa. Hawawezi kuona hatari zilizo jificha au mwisho wa kutisha wa njia wanayoiona kuwa ya furaha. Kwa njia ya kuzitimiza tamaa mbaya za chakula na ashiki pasipo kujizuia, nguvu zao hutupwa bure, na mamilioni huangamia ulimwenguni humu na kuukosa ulimwengu ujao. Wazazi wangekumbuka kuwa watoto wo hawana budi kuyapinga majaribu haya. Hata kabla ya kuzaliwa mtoto, matayarisho yangeanza, ambayo yatamwezesha mtoto kufaulu katika kupigana vita na yule mwovu.KN 158.5

    Ikiwa kabla ya kuzaliwa mtoto wake, mama mwenyewe ni mfisadi, kama ni mchoyo, mwenyewe harara, na mkali, tabia hizi zitaonekana kwa mtoto. Hivyo watoto wengi wamerithi mielekeo mibaya wasiyoweza kuishinda ila kwa shida sana.KN 159.1

    Lakini ikiwa mama hushika, bila kusitasita, kanuni njema, kama akiwa mwenye kiasi na mwenyewe kujizuia, kama ni mwenye utu wema, mpole, na mkarimu, aweza kumrithisha mtoto wake tabia hizo za thamani kuu.KN 159.2

    Watoto wachanga ni kioo kwa mama ambamo huweza kuona sura ya mazoea na mwenendo wake mwenyewe. Basi angejihadhari kama nini na maneno yake pamoja na mwenendo wake mbele ya hawa watoto wadogo! Tabia zo zote atakazo kuona wanazo hana budi kuwa nazo yeye mwenyewe.KN 159.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents