Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mambo ya Kuangalia kwa Mke Anayetazamiwa

  Mvulana na achague msichana atakayesimama imara kando yake ambaye ataweza kuchukua sehemu yake ya mzigo wa maisha, mke ambaye mvuto wake utamwadilisha mumewe na kumfanya safi, na ambaye kwa upendo wake atamfanya awe na raha.KN 131.1

  “Mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.” “Moyo wa mumewe humwamini ....Humtendea mema wala si mabaya, siku zote za maisha yake.” “Hufumbua kinywa chake kwa hekima, na sheria ya wema 1 katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; mumewe nave humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, lakini wewe umewapita wote.” Yeye apataye mke wa namna hiyo “apata kitu chema; naye ajipatia kibali kwa Bwana.”KN 131.2

  Hapa ni mambo yapasayo kufikiriwa: Je, yule unayekusudia kumwoa ataleta furaha nyumbani mwenu? Yu (mwanamke) mwangalifu, awezaye kutunza mali, ama akisha kuolewa, licha ya upeteza mapato yake, hata mali yako ataitawanya bure, huku akionyesha upendo wa juu iuu tu? Mwenendo wake ukoje wakati huu? Anacho kitu cho chote anachokitegemea wakati huu? Nafahamu kwamba mvulana ambaye amerukwa na akili kwa sababu va upendo na mawazo ya kuoa atayadharau maswali haya kana kwamba hayana maana wala manufaa yo yote. Lakini mambo haya yangefikiriwa sawasawa, maana yana matokeo katika maisha yenu ya wakati ujao.KN 131.3

  Katika kuchagua mke, peleleza tabia yake uijue. Je, atakuwa mstahimililivu na mwenye bidii ya kazi? Au atachoka kumtunza mama yako na baba yako wakati hasa wanapohitaji mwana aliye na nguvu wa kumtegemea? Je, atakutenga nao ili kuitimiza mipango na makusudi yake na kumfaa kwa anasa zake mwenyewe, na kuwatupa baba na mama ambao, badala ya kupata binti mpendwa watakuwa wamepotewa na mwana?KN 131.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents