Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Talanta Zako zafaa Hitaji Fulani

    Mungu ana nafasi kwa kila mmoja katika mpango wake mkuu. Talanta ambazo hazihitajiki hazitolewi. Talanta inayodhaniwa kuwa ni ndogo, Mungu ana mahali kwa ajili yake, nayo talanta hiyo moja, kama ikitumiwa kwa uaminifu, itafanya kazi ile ile ambayo Mungu ameikusudia iifanye. Talanta za kibarua zinahitajika katika kazi ya kuhubiri Injili nyumba kwa nyumba nazo zaweza kufanya makubwa zaidi katika kazi hii kuliko vipawa adimu. 4 9T31, 38;KN 75.1

    Watu wakitumia uwezo wao kama Mungu anavyoongoza, talanta zao zitaongezeka, uwezo wao utazidi, nao watakuwa na hekima itokayo mbinguni katika kutafuta kuwaokoa waliopotea. Lakini washiriki wa kanisa wakiwa walegevu na wasio waangalifu wa madaraka yao waliyopewa na Mungu kuwahudumia wengine, wawezaje kutazamia kupokea hazina ya mbinguni? Wenye kujidai kuwa Wakristo wasipoona mzigo moyoni kuwaangazia wale walio gizani, wakikoma kutoa neema na maarifa, wanapungukiwa ufanamu, wanapoteza hali ya kuyathamini majaliwa makubwa ya mbinguni; na kwa kukosa kuyathamini wao wenyewe, wanashindwa kutambua umuhimu wa kuyapeleka kwa wengine kwa wengine.KN 75.2

    Tunaona makanisa makubwa katika mitaa mbalimbali. Washiriki wake wamepata ujuzi mkubwa wa Neno la Mungu, na wengi wanaridhika kulisikia Neno la uzima bila kujaribu kuwatolea wengine nuru. Hawaoni moyoni wajibu uwapasao kwa ajili ya maendeleo ya kazi hii, wanashauku ndogo sana juu ya wokovu wa roho za watu. Wamejawa na bidii katika mambo ya anasa za dunia, lakini dini yao haionekani katika shughuli zao. Wanasema: “Dini ni dini, na shughuli ni shughuli.” Wanaamini kwamba kila moja ina nafasi yake sawasawa, lakini husema: “acha yatengwe.”KN 75.3

    Kwa sababu ya nafasi zisizojaliwa na kutumia vibaya majaliwa na bahati walizo nazo, washiriki wa makanisa haya hawakui “katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo” (2 Petro 3:18). Kwa hiyo ni wadhaifu katika imani, wapungufu wa ujuzi na watoto katika mambo ya maisha. Hawana mizizi wala msingi katika Neno la Mungu. Kama wakiendelea hivi, madanganyifu mengi ya siku za mwisho yamkini yatawadanganya, maana hawatakuwa na macho ya kiroho kupambanua kweli na kosa. 5 67424, 425;KN 75.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents