Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 9 - Vitabu na Magazeti ya Kanisa Hili

    KAZI yetu ya kuchapisha vitabu ilianzishwa kwa uongozi wa Mungu chini ya uangalizi wake maalum. Ilikusudiwa kutimiza kusudi halisi. Waadventista Wasabato wamechaguliwa na Mungu kuwa watu wa pekee, waliotengwa na walimwengu. Kwa ufa mkubwa wa Neno la kweli amewatenga na chimbo la mawe la walimwengu na kuwaunganisha naye Mwenyewe. Amewafanya wajumbe wake na amewaita mawakili wake katika kazi ya mwisho ya wokovu. Amana kubwa kabisa ya kweli waliyopata kuaminiwa wanadamu, maonyo mazito sana ya kutisha ambayo yapasa kupelekewa binadamu kutoka kwa Mungu, yamekabidhiwa kwao ili wawapelekee walimwengu; na katika kuitimiza kazi hii nyumba zetu za kuchapisha vitabu ni miongoni mwa njia za kufaa sana.KN 83.1

    Vitabu na magazeti yatolewayo kutoka nyumba zetu za kuchapisha hayana budi kuwatayarisha watu kuonana na Mungu. 17T 138, 139;KN 83.2

    Ikiwako kazi moja yenye maana zaidi ya nyingine, kazi hiyo ni ile ya kuvieneza vitabu na magazeti yetu kwa watu na kwa njia hii kuwaongoza kuyachunguza Maandiko. Kazi ya utume kuingiza vitabu na magazeti yetu nyumbani mwa watu, kuuza vitabu, na kusali nao na kuwaombea kwa Mungu ni kazi njema na mojawapo ambayo itawaadilisha wanaume na wanawake kufanya kazi ya uchungaji. 24T 390;KN 83.3

    Uuzaji wa vitabu vyetu ni aina ya kazi ya uinjilisti iliyo kubwa na yenye faida sana. Vitabu vyetu vyaweza kwenda mahali ambapo mikutano haiwezi kufanywa. Mahali kama hapa mwinjilisti wa vitabu huwa badala ya mhubiri. Kwa kazi ya kuuza vitabu ukweli hutolewa kwa maelfu ambao isingekuwa hivyo kamwe wasingeusikia.KN 83.4

    Wainjilisti wa vitabu hawana budi kwenda kwenye sehemu mbalimbali za nchi. Ukubwa wa kazi hii hulingana kabisa na ule wa kazi ya uchungaji. Mhubiri na mjumbe aliye kimya, wote wawili hutakikana kwa kuifanya na kuitimiza kazi kuu iliyo mbele yetu. 3 CM 8; KN 83.5

    Mungu ameweka kazi ya uinjilisti wa vitabu kama njia ya kuwatolea watu nuru iliyomo vitabuni mwetu, na wainjilisti wa vitabu wangevutwa na ukubwa wa kuleta mbele ya walimwengu upesi iwezekanavyo vitabu vilivyo muhimu kwa ajili ya mafundisho yetu na kwa kuwapatia nuru ya kiroho. Hii ndiyo kazi hasa ambayo Mungu apenda watu wake waifanye wakati huu. Wote wanaojitoa wakfu kwa Mungu kufanya kazi kama wainjilisti wa vitabu wanasaidia kutoa ujumbe wa mwisho wa onyo kwa walimwengu. Si kwamba tunaithamini kazi hii kupita inavyostahili; maana isingekuwa kwa ajili ya jitihada za mwinjilisti wa vitabu, wengi kamwe wasingelisikia onyo hili. 46T 313 KN 83.6

    Yapasa vitabu na magazeti yetu kuenea kila mahali. Hebu yatolewe katika lugha nyingi. Ujumbe wa malaika wa tatu umepasa kutolewa kwa njia hii na kwa njia ya mhubiri. Ninyi wenye kuuamini ukweli kwa wakati huu, amkeni. Ni wajibu wenu sasa kuingiza njia zote iwezakanavyo kuwasaidia wale wanaolifahamu Neno la Mungu kulihubiri. Sehemu ya fedha ipatikanayo kwa kuuza vitabu na magazeti yetu yapasa kutumiwa kuongeza vifaa vyetu ili kuzidisha vitabu na magazeti zaidi ambavyo vitafumbua macho na kuutayarisha udongo wa moyo. 59T 62;KN 84.1

    Nimeamuriwa kwamba hata mahali watu wanapousikia ujumbe huu kutoka kwa mhubiri, mwinjilisti wa vitabu angeendelea na kazi yake akishirikiana na mhubiri; maana ingawa mhubiri aweza kuutoa ujumbe huu kwa uaminifu, watu hawawezi kuushika wote. Hivyo kitabu ni kitu cha maana, licha ya kuwaamsha waone ukubwa wa Neno la Mungu kwa wakati huu, hata kuwafanya watie mizizi na kuwa na msingi katika ukweli na kuimarishwa katika kushindana na makosa ya udanganyifu. Magazeti na vitabu ni njia za Bwana Mungu za kuweka daima ujumbe kwa ajili ya wakati huu mbele za watu. Katika kutia nuru na kuziimarisha roho za watu katika Neno la Mungu, vitabu na magazeti vitafanya kazi iliyo kubwa zaidi ya ile iwezayo kufanywa kwa kulihubiri Neno peke yake. Wajumbe wa kimya ambao huwekwa nyumbani mwa watu kwa njia ya kazi ya mwinjilisti wa vitabu watayatia nguvu mahubiri ya Injili kwa kila njia; maana Roho Mtakatifu ataichoma mioyo ya watu wakivisoma vitabu, sawa na anavyoichoma mioyo ya wale wanaoyasikiliza mahubiri ya Neno la Mungu. Huduma ile ile ya malaika hutumika kwa vitabu vyenye ukweli kama inavyotumika katika kazi ya mhubiri. 66T 315, 316 KN 84.2

    Mipango ya busara na ifanywe kuwasaidia wanafunzi wanaostahili kujipatia gharama zao za Shule kwa kuviuza vitabu hivi, kama wakipenda. Wale ambao hujipatia fedha ya kutosha kwa njia hii hulipa gharama zao za shule katika vyuo vyetu wanamofundishwa watenda kazi watajipatia maarifa ya kufaa yenye maana sana ambayo yatawasaidia kwa kazi ya utume mahali papya katika nchi zingine. 79T 79;KN 84.3

    Washiriki wa kanisa wakifahamu ukubwa wa kuvieneza vitabu na magazeti yetu, watatumia wakati zaidi kwa kazi hii.” 8 CM 7;KN 85.1

    Kadiri muda wa kuangaliwa kama twafaa au hatufai unavyoendelea, patakuwako nafasi kwa mwinjilisti wa vitabu kufanya kazi. 96T 478;KN 85.2

    Ndugu na dada, Mungu atapendezwa kama mtashikilia kwa moyo kusaidia nyumba ya kuchapisha vitabu kwa sala zenu na kwa mali zenu. Ombeni kila siku asubuhi na jioni ili ipate kupokea mbaraka mkubwa wa Mungu. Msitie nguvu lawama na manung’uniko. Manung’uniko na malalamiko yasitoke midomoni mwenu; kumbukeni kuwa malaika huyasikia maneno hayo. Wote hawana budi kuongozwa kuona kuwa nyumba hizi za kazi zimewekwa na Mungu. Wale wanaozivunjia heshima ili kujipatia faida wao wenyewe itawabidi kutoa hesabu kwa Mungu. Mungu anakusudia kwamba kila kitu kihusucho kazi yake kitendewe kama kitakatifu. 107T 182, 183KN 85.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents