Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Vyombo vya Nyumbani Viwe Vyepesi Visivyo vya Bei Kubwa

    Weka nyumbani mwako vyombo vyepesi, rahisi kutengenezwa, vitu ambavyo vitastahimili kutumiwa, viwezavyo kusafishwa kwa urahisi, na rahisi kupatikana, visivyo vya bei kubwa. Kwa kujaribujaribu, waweza kuifanya nyumba isiyo na vitu vya bei kubwa kuwa ya kupendeza na kuvutia macho, kama pakiwako upendo na moyo wa kuridhika. Raha haipatikani katika mambo ya kujionyesha tu. Utaratibu wa mambo ya watu wa nyumbani ukiwa mwepesi ndivyo nyumba hiyo itakavyozidi kuwa ya furaha. Si lazima kuwa na mastakimu na vyombo vya gharama kubwa kusudi kuwaridhisha watoto na kuwapendeza nyumbani kwao, lakini ni jambo la muhimu kuwaonyesha upendo na malezi mazuri. 1131-155;KN 170.5

    Mnapaswa siku zote kushirikikiana mali nyumbani mwenu. Kumbukeni kuwa mbinguni hakuna machafuko, na ya kuwa nyumba yenu ingekuwa kama mbinguni mkiwa bado mngali hapa chini. Kumbukeni kuwa kwa kufanya kwa uaminifu siku kwa siku mambo yale madogo madogo ya kufanywa nyumbani, mwatenda kazi pamoja na Mungu, mkithibitisha tabia ya Kikristo. Kumbukeni wazazi, kwamba mnauhudumia wokovu wa watoto wenu. Ikiwa mazoea yenu ni safi, yasiyo na makosa, kama mwaonyesha umaridadi na utaratibu, sifa nzuri na haki, utakaso wa roho, mwili na moyo, mwayatii maneno ya Mkombozi, “Ninyi ni nuru ya ulimwengu.”KN 171.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents